Jumapili 27 Aprili 2025 - 06:43
Mwanazuoni wa kisuni Lebanon ashangazwa na msimamo wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo; Lebanon Haitakuwa Makazi ya Wazayuni

Sheikh Ahmad al-Qattan ameeleza kushangazwa kwake na hatua iliyo chukuliwa na wizara ya mambo ya nje ya Lebanon kwa kumuita balozi wa Iran, na akasema: Balozi wa Iran anatetea uwezo wa Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad al-Qattan, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya "Qawluna wal-Amal" ya Lebanon, katika hotuba yake ya kila wiki ya kisiasa katika mji wa Bar Elias ulioko katika eneo la Bekaa, alieleza kushangazwa kwake kuhusiana na hatua ya wizara ya mambo ya nje ya Lebanon kwa kumuita Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na akasema: Balozi wa Iran anatetea silaha na uwezo wa Lebanon.

Akaongeza kwa kuashiria: Mabalozi wa nchi mbalimbali huzunguka huku na kule, huja na kuingilia masuala ya ndani. Baadhi ya maafisa wa serikali ya Marekani hutangaza wito wa mahakama na maamuzi mengine. Je, hiyo siyo kuingilia? Amerika haiingilii mambo ya Lebanon? Ufaransa haiingilii mambo ya Lebanon? Je, serikali zote za kibepari hazingilii masuala ya Lebanon?!

Sheikh al-Qattan aliweka wazi kwa kusema: Kwa sababu tu balozi mmoja Mwislamu aliandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba: "Lebanon haipaswi kukabidhi silaha ilizonazo ili isiwe shabaha kwa Wazayuni," waziri alipaza sauti na kusema; balozi huyo asijaribu kuzungumza kuhusu heshima na uwezo wa Lebanon.

Akasema kwa kusisitiza kuwa Lebanon kamwe haitakuwa makao au njia ya Wazayuni: Nchi hii ni mali ya watoto wake, watu wake, familia zake, na kila mtu anayependa nchi hii na anataka ibaki imara mbele ya maadui zake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha