Jumanne 22 Aprili 2025 - 10:25
Ulinganisho wa Kuvutia uliofanywa na Rais wa Colombia kati ya Wapalestina na Nabii Issa (amani iwe juu yake)

Rais wa Colombia, Gustavo Petro, katika hotuba yake siku ya Ijumaa, alilinganisha hali ya mateso wanayo ipotia Wapalestina na simulizi ya maisha ya Nabii Issa Masih (amani iwe juu yake).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Rais Gustavo Petro, siku ya Ijumaa katika hotuba yake, alilaani vikali vitendo vinavyo fanywa na utawala haramu wa Israel huko Ghaza na kuifananisha hali ya mateso wanayoipitia Wapalestina na mateso aliyo yapitia Nabii Isa Masih (amani iwe juu yake).

Raisi Petro, alipokuwa akijibu ujumbe kuhusiana na Daktari Hossam Abusafiyah daktari mashuhuri wa Kipalestina aliyekamatwa na utawala wa Kizayuni, alisema:  
"Tuangalie na kutafakari nyakati za maumivu na mateso aliyopitia Nabii Isa Masih ndani ya mauaji ya kimbari ya kikatili na yenye kumwaga damu yanayofanywa na Israel huko Ghaza, pamoja na masaibu ya watu wanyonge katika eneo hilo."

Daktari Abusafiyah ambae alikuwa mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Ghaza, ambaye alikamatwa na majeshi ya Israel mapema mwaka huu.

Taasisi za haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari vya ndani vimekuwa vikitoa onyo kali kuhusu kuzorota kwa hali yake katika wiki za hivi karibuni. Hata hivyo, bado anazidi kufanyiwa vitendo vya kikatili na kupewa mateso.

Petro alitoa hotuba hii wakati wa Wiki Takatifu ya Wakristo, na alisisitiza umuhimu na utakatifu kwa kipindi hicho. Rais huyo wa Colombia amekuwa mstari wa mbele na mkosoaji wa muda mrefu wa jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha