Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Majlisi ya umoja wa Waislamu wa Pakistan kwa kuandaa kongamano hili la adhimu lililopewa jina la “Karbala ya zama za Palestina”, kwa mara nyingine tena imesisitiza msimamo wake thabiti wa kuwaunga mkono watu wanyonge wa Palestina. Katika hafla hiyo, shakhsia mashuhuri za kisiasa, kidini na vyombo vya habari kutoka madhehebu mbalimbali walihudhuria na kusisitiza juu ya umoja na mshikamano wa umma wa kiislamu kwenye kuwatetea watu wa Palestina.
Seneta Raja Nasir Abbas Jafari, mwenyekiti wa Majlisi ya umoja wa waislamu wa Pakistan, katika hotuba yake alizungumza bayana kwamba kuunga mkono taifa la Palestina linalodhulumiwa ni "wajibu wa kisheria, kimaadili na kibinadamu."
Aliendelea kusema kwamba: “Maadui wanajaribu kuzima mwangaza wa muqawama, lakini sisi tuna wajibu wa kuuendeleza na kuuimarisha mwangaza huo; kwani Mwenyezi Mungu ameahidi kuwasaidia wale wanaoisaidia dini yake.”
Seneta Raja Nasir Abbas, kwa kunukuu ujumbe wa Ashura, aliongezea kuwa: “Yazid wa jana alishindwa, na Yazid wa leo pia yupo kwenye hukumu ya kushindwa. Kushikamana na misingi ya haki ndio siri ya ushindi wa kweli. Kama ambavyo wanawake wa Ahlul Bayt waliutangaza kwa ujasiri ujumbe wa haki kwa walimwengu baada ya tukio la Karbala, vivyo hivyo leo hii tunahitaji kujitolea na ujasiri kwa kiwango hicho hicho.”
Mushtaq Ahmad Khan, seneta wa zamani wa Pakistan, pia alihutubia hafla hiyo huku akikosoa vikali ukimya wa nchi za kiislamu, na kusema: “Leo hii Yemen na Iran wamesimama pamoja na Palestina, nasi pia tuko nyuma yao kuwasaidia. Tunaitaka serikali ya Pakistan imfukuze balozi wa Marekani, ipige marufuku bidhaa za Wazayuni, na ianze kuwaunga mkono watu wa Palestina kwa vitendo.”
Mwishoni mwa hafla hiyo, Fakhr Abbas, mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Imamiya, huku akiwatukuza mashujaa waliouawa katika njia ya muqawama, alisema: “Marekani, ambayo daima imekuwa ikijinasibisha kuwa mtetezi wa haki za binadamu, leo hii kwa kunyamazia mauaji ya kinyama yanayoendelea Ghaza, imeonesha sura yake halisi. Ikiwa leo hii kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza kusemwa kuwa ni mtetezi wa kweli wa ubinadamu, bila shaka mtu huyo ni Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei. Tunatuma salamu zetu za heshima kwa mashahidi wote wa muqawama.”
Maoni yako