Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza: Imepokewa kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba alisema: Jibril aliteremka kwa Nabii Adam (a.s.) na akamwambia: “Ewe Adam, nimeamrishwa nikukhiyarishe moja kati ya vitu vitatu. Chagua kimoja na uache viwili vingine.” Adam (a.s.) akamuuliza: “Ewe Jibril, hivyo vitatu ni vipi?” Jibril akajibu: “Ni akili, haya na dini.” Adam (a.s.) akasema: “Nimechagua akili.” Jibril akaviambia haya na dini: “Ondokeni na muiache akili.” Haya na dini vikasema: “Ewe Jibril, sisi tumeamrishwa kuwa popote akili ilipo, nasi tuwepo pamoja nayo.”
Jibril akasema: “Hivyo basi, endeleeni kuwa pamoja,” kisha akaondoka.
(Rejea: Usul al-Kafi, Juzuu ya 1, uk. 10)
Katika riwaya nyingine imepokewa hivi:
Imepikewa kutoka kwa Abi Ja'far (a.s.) amesema: Wakati Mwenyezi Mungu alipoiumba akili, aliitamkisha, kisha akaiambia: “Njoo mbele,” ikaja mbele. Kisha akaiambia: “Rudi nyuma,” ikarudi nyuma. Kisha akasema: “Naapa kwa utukufu wangu, sikuumba kiumbe chochote ambacho ni kipenzi zaidi kwangu kuliko wewe, ewe akili. Na wala Sikukamilisha isipokuwa kwa yule ninayempenda. Hakika mimi kupitia wewe ninaamuru, na ninakataza, ninatoa thawabu, na ninaadhibu.”
(Rejea: Wasāil al-Shīʿah, Juzuu ya 1, uk. 39).
Maoni yako