Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Maulamaa wa kiislamu nchini Lebanon, katika taarifa iliyotolewa baada ya kikao chao cha kila mwezi, limezitaka nchi za kiarabu na kiislamu pamoja na majeshi yao yenye mamilioni ya wanajeshi kuchukua hatua za haraka kuwasaidia waislamu wa Palestina, hususan walioko Ghaza.
Baraza hilo limeeleza kuwa watu wa Palestina na Gaza, wanakabiliwa na vita vya maangamizi na wala si mateso ya kawaida, na hivyo limekemea vikali kuendelea kwa matamko ya kulaumu na kulaani bila kuchukua hatua halisi.
Baraza hili limeweka wazi kuwa: “Kuhalalisha uhusiano wa kawaida na adui Mwisraeli si sehemu ya mafundisho ya dini yetu. Suluhisho la kweli ni kwamba mvamizi aondoke kabisa katika ardhi yote ya Palestina, kwa kuwa Palestina ni ardhi takatifu kwetu, ambapo tunahifadhi bendera ya uongozi wa misikiti miwili mitukufu, Qibla mbili, na uangalizi wa Msikiti Mkuu na Msikiti wa Al-Aqsa wa Mtume Mtukufu (s.a.w).”
Baraza hilo pia limesisitiza kuwa: “Leo maeneo ya Shamat yanahitaji vifaa, fedha, chakula na uungwaji mkono wa kisiasa unaompendeza Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kwa zaidi ya miaka themanini, tumekuwa tukiomba msaada kutoka kwa taasisi za kimataifa hasa jamii ya kimataifa, lakini yote hayo yamekuwa ni sawa na kupoteza muda na haki zetu.”
Maoni yako