Jumamosi 19 Aprili 2025 - 17:49
Bendera ya Palestina yainuliwa kwenye mahafali iliyo fanyika chuo kikuu cha Harvard

Bendera za Palestina zimeinuliwa kwenye sherehe ya mahafali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard.

Kwa mujibu wa ripoti ya kikundi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ikinukuu kutoka katika gazeti la "Middle East Monitor", bendera za Palestina zimeinuliwa kwenye sherehe ya kuhitimu masomo chuo kikuu cha Harvard.

Hili linajiri huku chuo kikuu cha zamani zaidi nchini Marekani kikiwa ndicho chuo cha kwanza kukataa mapendekezo ya kisera ya serikali ya Trump iliyolenga kupunguza au kukandamiza shughuli za wanafunzi na wanachuo walioko katika hali ya mshikamano na Palestina, jambo ambalo huenda likaleta changamoto kwa chuo hiki katika kupata ufadhili wa dola bilioni 2 kutoka kwenye serikali ya shirikisho siku za usoni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha