Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Bwana Khalid bin Salman, waziri wa ulinzi wa Saudi Arabia, alasiri ya leo alivyo onana na kiongozi mkuu wa mapinduzi ya kiislamu, aliwasilisha ujumbe wa Mfalme wa nchi hiyo kwa Hadhrat Ayatullah Khamenei.
Kiongozi mkuu wa mapinduzi ya kiislamu katika mazungumzo hayo alisisitiza kuwa: "Imani yetu ni kuwa uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia ni wenye manufaa kwa pande zote mbili, na mataifa haya mawili yanaweza kukamilishana."
Hadhrat Ayatullah Khamenei huku akisisitiza kwamba, kuimarika kwa mahusiano ya mataifa haya mawili kuna uadui, alibainisha: Lazima tuvishinde vikwazo hivi vya uadui, na sisi tuko tayari kuhusu jambo hili.
Yeye, akigusia baadhi ya maendeleo ya Iran, alisema: "Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuisaidia Saudi Arabia katika nyanja hizi."
Kiongozi mkuu wa mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza: "Jambo la udugu, kushirikiana, na kusaidiana ni bora zaidi mno kuliko kuyategemea mataifa mengine.
Maoni yako