Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatullah Jawadi Amuli katika maandishi yanayo husu mafundisho na mafunzo yanayopatikana kutokana na kuhudhuria makaburini, amesema:
“Mtu huenda makaburini kwa ajili ya kuwaombea wazazi wake maghfira (msamaha), au kwa ajili ya yeye mwenyewe kujifunza jambo fulani? Amesema: Waombee wazazi wako maghfira, waombee maghfira waumini, kwani unaposoma "Surat al-Hamd", na aya na nyenginezo, yote hayo ni kwa ajili yao. Lakini pia wewe mwenyewe omba dua, zungumza nao, waapize, waambie: ‘Ninakuapisheni kwa "Lā ilāha illallāh", niambieni huko kuna habari gani?’ Hii maana yake ni nini?
«يَا أَهْلَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ بِحَقِّ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ كَيْف وَجَدْتُم قَوْل لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ مِنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ؟»
Enyi «أَهْلَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ», ninakuapisheni kwa «لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ», niambieni huko kuna habari gani?
Hii ni madarasa. Mtu akienda makaburini kisha akarejea bila ya kujifunza chochote hiyo ni hasara.”
Maoni yako