Jumamosi 19 Aprili 2025 - 17:47
Utambulisho wa kiuwanafunzi wa dini (talaba) ni Lulu ya asili kwa mwanafunzi

Mkurugenzi wa Hawzah nchi Irani, katika kikao chake na wanafunzi wa Hawzah kilichofanyika katika mji wa Tehran – Iran, alielezabkuwa: Neema kuu zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kuwepo katika uwanja wa dini pamoja na kuiongoza jamii.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah A’rafi, mudiri wa Hawzah nchini kote pamoja na wasaidizi wake, katika kikao na wanafunzi wa Hawzah kilichofanyika jijini Tehran, alisema: Neema kuu zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kuwepo katika uwanja wa dini pamoja na kuiongoza jamii.

Ayatollah A’rafi aliongeza: Wale ambao wameonja ladha tamu ya kuwa wanafunzi na wapiganaji kwa ajili ya Imam wa Zama (a.s), hawata ibadilisha fahari hiyo na kitu chochote kile kingine. Hawzah katika zama hizi mpya imebeba majukumu yasiyo na kifani mabegani mwake. Majukumu hayo hayakuwahi kuwasilishwa hapo kabla katika historia ya Hawzah kwa namna hii wala kwa upeo huu.

Akiashiria kuwa Hawzah imepitia njia ngumu katika historia yake, alisema: Katika historia mambo mengi makubwa yameweza kupatiwa ufumbuzi kupitia Hawzazah, na fahari nyingi zimeandikwa na wapiganaji wa Imam wa Zama (ajjalallahu farajahu). Hawzah ilianzia kutoka Madina, kisha ikaelekea Najaf, Baghdad, Kufa, Qom na Ray, na katika njia hii, mafakihi na watu mashuhuri waliweza kulihifadhi jina kubwa la Hawzah.

Mudiri wa vyuo vya dini (Hawzah) nchini kote Irani, kwa kueleza kwamba historia ya Hawzah imeambatana na kupanda na kushuka, alisisitiza kuwa: Mashahidi wameweza kuendeleza njia hii hadi kufikia zama za mapinduzi ya kiislamu. Mapinduzi haya yametoa takriban mashahidi elfu tano kutoka katika Hawzah kwa ajili ya uislamu. Sisi talaba (wanafunzi wa dini) ni warithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) na Amirul-Muuminin (a.s), ambao maisha yao waliyatumikia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na uislamu.

Akiashiria historia ya Hawzah katika elimu, maadili, malezi, kutatua matatizo ya watu, na siasa, alisema: Historia hii tukufu imepelekea kuwa kiongozi mkuu wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran naye pia ajihesabu kuwa ni talaba (mwanafunzi wa dini). "Utambulisho wa kitalaba ni lulu ya asili kwa talaba". Iwapo lulu hii ya msingi itahuishwa, basi tutashuhudia kujitokeza kwa shakhsia kubwa mno katika chuo cha dini (Hawzah).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha