Shirika la Habari la Hawza - Picha ya kijana mdogo wa Kipalestina ambaye mikono yake yote miwili ilikatwa kufuatia shambulio la Israel dhidi ya Ghaza, katika siku ya Alhamisi ilichaguliwa kuwa picha bora zaidi iliyo chapishwa duniani kwa mwaka 2025.
Abu Al-Wafa, katika tamko lililotolewa na Jumuiya ya kimataifa ya Wapiga Picha wa Habari, alisema: “Mojawapo ya mambo magumu zaidi ambayo mama yake Mahmoud alinihadithia ilikuwa ni namna ambapo Mahmoud, kwa mara ya kwanza alipotambua kuwa mikono yake imekatika, alizungumza na mama yake, na sentensi ya kwanza kabisa aliyomwambia ilikuwa: ‘Sasa nitakukumbatia vipi?’”
Mshindi wa mashindano haya ya heshima ya 68 ya upigaji picha wa habari alichaguliwa kutoka miongoni mwa washiriki 59,320, ambapo kazi zao zilitumwa na wapiga picha 3,778 kutoka nchi 141 ziliamuliwa na jopo la majaji.
Maoni yako