Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Shafqat Shirazi, ambaye ni katibu wa masuala ya kigeni wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, alitoa taarifa rasmi kulaani vikali tukio hilo la kikatili nchini Nigeria katika Siku ya Quds, na kuhimiza jamii ya kimataifa kulaani ukiukwaji huo wa wazi wa haki za binadamu.
Katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaliyofanyika Nigeria tarehe 30 Machi 2025, vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo vilifyatua risasi moja kwa moja kwa waandamanaji, na kuua watu 10 huku wengine wengi wakijeruhiwa au kukamatwa. Hadi sasa, hakuna taarifa yeyote iliyotolewa kuhusu hali ya waliokamatwa, na vyombo vya habari vya kimataifa havijatoa msimamo wowote kuhusu tukio hilo la umwagaji damu.
Hujjatul-Islam Shafqat Shirazi, katika kulaani kwake tukio hilo, aliikosoa vikali taasisi za haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari vya kimataifa kutokana na ukimya wao huku akisema, akisema: “Kama ilivyo desturi kila mwaka, mwaka huu pia watu walikusanyika kwa amani kuonyesha kuwaunga mkono watu wa Palestina na kulaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, lakini walikumbana na ukatili wa jeshi la Nigeria.”
Aliongeza kuwa: “Hatua hii ya kijeshi siyo tu kuwa ni kinyume cha sheria, bali pia ni ya kinyama na isiyo ya kibinadamu. Ni wajibu wa kila Muislamu duniani kutokaa kimya mbele ya dhulma hii ya wazi, bali wazungumze kwa sauti moja na kuiambia dunia ukweli.”
Maoni yako