Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A'arafi, Mkuu wa Vyuo vya dini ya Kiislamu Iran, kwa kutoa tamko la kukemea mauaji ya kikatili ya watu wasio na hatia nchini Syria kwa mikono ya vikundi vya kijeshi vya Tahrir al-Sham, aliwasihi Ulamaa wa kiislamu kutoka duniani kote pamoja na viongozi wa dini nyingine kwamba, waweke wazi msimamo wao dhidi ya vitendo hivi visivyo halali, na wajiunge katika kupinga kwa dhati na kuyasihi mashirika ya kimataifa na asasi za haki za binadamu zichukue hatua kwa ajili ya kutatua vitendo vya uhalifu wa kivita nchini Syria.
Maelezo ya tamko lake ni kama ifuatavyo:
Bismillahir Rahmanir Rahim:
"Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki, na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake, lakini asipite mpaka katika kuuwa, kwani yeye anasaidiwa (Quran, Surah Al-Isra, Ayah 33).
Uislamu ni dini inayosisitiza sana uhifadhi wa maisha, mali, na heshima ya binadamu, haukubali mauaji ya wasio na hatia. Na Mwenyezi Mungu, Mtukufu na Mjuzi, ameeleza wazi katika Qur'an: "Usiue nafsi aliyokataza Allah isife ila kwa haki" (Surah Al-Isra, Ayah 33).
Aya hii inasisitiza uharamu wa kuuawa kwa binadamu, hasa wale wasio na hatia. Hivyo basi; vitendo vyovyote vya kuangamiza maisha ya watu wasio na hatia, hasa kama tunavyoshuhudia huko Syria, ni kinyume cha mafundisho ya kidini.
Mauaji ya watu wa Syria kupitia vikundi vya kijeshi vya Tahrir al-Sham sio tu kinyume na misingi ya Kiislamu bali pia yanachochea mgawanyiko na kuathiri jamii ya Kiislamu.
Kulingana na sheria za kimataifa za haki za binadamu, ikiwemo Mikataba ya Geneva na Makubaliano ya Kimataifa ya Haki za Kiraia na Kisiasa, mauaji ya wasio na hatia na vitendo vyovyote vya vurugu vinavyofanywa dhidi ya watu wa kawaida, hasa watoto, wanawake, na raia, vinalaaniwa vikali.
Kifungu cha 3 cha Mikataba ya Geneva kinachohusiana na vita na mapigano ya kijeshi kinahitaji kwamba vita vifanyike kwa misingi ya sheria za kibinadamu na kinakataza mashambulizi dhidi ya raia. Kuikiuka kwa misingi hii, kama inavyoshuhudiwa katika matendo ya vikundi kama Tahrir al-Sham, ni uhalifu wa kivita na unastahili kuchukuliwa hatua katika majukwaa ya kimataifa.
Naviomba vikundi vyote vya kijeshi nchini Syria kulazimiana na misingi ya Kiislamu na kibinadamu na kujiepusha na vurugu pamoja na mauaji ya wasio na hatia. Katika kipindi hiki kigumu ambapo Shetani mkubwa Marekani, na dhalimu wake utawala wa Israel wauwaji wa watoto uonajaribu kuudhuru Uislamu wa kweli, njia pekee ya kumaliza mgogoro wa Syria ni juhudi za kuleta amani na umoja wa kitaifa. Ujumbe wa Uislamu daima ni ujumbe wa amani, utulivu, na umoja. Aya na hadithi za Kiislamu zinatufundisha kuwa lengo la vita na migogoro yoyote lazima liwe ni kuleta amani na usalama, na wala sio mauaji ya wasio na hatia.
Natoa salamu zangu za rambi rambi kwa huzuni kubwa kutokana na mauaji ya kikatili ya wasio na hatia huko Syria, napinga vikali vitendo hivi na nawasihi Ulamaa wa Kiislamu na viongozi wa dini nyingine kukemea vitendo hivi visivyofaa na kuonyesha msimamo wao. Nayaomba mashirika ya kimataifa na asasi za haki za kibinadamu zichukue hatua halisi na za dharura ili kumaliza uhalifu wa kivita huko Syria na kuwafikisha wahusika katika vyombo vya sheria vya kimataifa.
Na amani zitakuwa kwa wale wanaofuata uongofu.
Ali Reza A'arafi
Maoni yako