Jumanne 4 Machi 2025 - 14:57
Imamu wa Ijumaa wa Baghdad: Upinzani dhidi ya Israel hauishi (haukamiliki)

Hawza / Ayatollah Sayyid Yassin Mousawi, Imamu wa Ijumaa wa Baghdad akiashiria kuhusiana na Mazishi na Maziko Matukufu ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah amemtaja kuwa ni "Shahidi wa Ummah" na kusisitiza kuwa, Muqawamah (Upinzani) dhidi ya Israel licha ya kuwepo tofauti kubwa za vifaa (vya kijeshi), umeweza kuibua ukweli (uhalisia) mpya katika eneo la Kikanda.

Kwa mujibu wa huduma ya Kimataifa ya Shirika la habari la "Hawza", Ayatollah Sayyid Yassin Mousawi, Imam wa Swala ya Ijumaa huko Baghdad, akizungumzia mazishi na maziko matukufu ya Kiongozi wa Upinzani (Muqawamah) wa Kiislamu nchini Lebanon, Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alimwita kuwa ni "Shahidi wa Ummah".

Ameongeza kuwa: Mazishi ya Sayyid Hassan Nasrallah huko Beirut yalikuwa ni tukio muhimu lililoonyesha nafasi na hadhi ya shakhsia huyo mkubwa katika uongozi wa mhimili wa mapambano dhidi ya Israel.

Ayatollah Mousawi amesema: Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah aliongoza harakati kubwa ya Muqawamah iliyojumuisha Palestina, Lebanon, Syria, Iraq, Yemen na hata maeneo mengine.

Ameongeza kuwa: Licha ya kuwepo tofauti kubwa katika vifaa na suhula za Muqawamah ukilinganisha na vikosi vya Israel na Marekani, Upinzani (Muqawamah) huo umeweza kuibua ukweli (uhalisia) mpya katika eneo la kikanda.

Ayatollah Mousawi aliendelea kusema: Vita hivyo si vita vya silaha na zana, bali ni vita vya irada na imani. Shahidi Nasrallah alijua kwamba hakuna usawa kati yetu na Marekani na Israel katika suala la silaha za kivita au teknolojia, lakini alithibitisha kwamba iarada na imani vinaweza kuleta ushindi.

Profesa mashuhuri wa Seminari (Hawza) ya Najaf al-Ashraf alisema: Licha ya kuuawa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, vita dhidi ya Israel havijaisha na umma wa Kiislamu na Waarabu bado una uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha