Kwa mujibu wa kundi la Tarjama la Shirika la Habari la Hawza, Tarjama na taswira (picha) ya maandishi ya hotuba ya Shahidi Safiyyu al-Din ambayo ilitakiwa kutolewa naye siku hiyo hiyo alipouawa Shahidi katika shambulio la anga la utawala wa Kizayuni, ni kama ifuatavyo:
(“Hakika ni suala lililokuwa bayana kwenu katika maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), ambapo alikuwa mfano mzuri kwa wale wanaotaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama na kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi. (Lakini) Waumini walipoliona jeshi la makundi walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli.
Na suala hili halikuwazidishia ispokuwa imani na utii. Miongoni mwa Waumini kuna watu waliosimama kwa (ukweli na) uaminifu juu ya (ahadi) agano walilofanya na Mwenyezi Mungu; Wengine walishikamana na agano lao hadi mwisho (na wakiwa katika njia hiyo wakanywa katika kinwaji cha Kifo cha Kishahidi), Na wengine bado wanangojea; Na wala hawakubadili - ahadi - agano lao." (Surah Ahzab, Aya ya 21-22-23)
Awali ya yote napenda kutoa pole zangu za dhati kwa Familia za Mashahidi, na pole kwa majeruhi na wahanga wa hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awalipe subira yao.
Ninazungumza nanyi wapendwa katika nchi yetu tuipendayo ya Lebanon, pamoja na nchi za Kiarabu na Kiislamu, na watu huru wa duniani na wale wote wasiokubali kudhulumiwa na kupigana dhidi ya Madhalimu.
Hapana shaka kwamba huzuni na majonzi kutokana na jinai na mauaji yanayofanywa na adui Mzayuni yameweka kivuli katika nyoyo zetu. Jinai hizi zimekuwa zikifanywa chini ya kivuli cha uungaji mkono wa Marekani na kimya cha kimataifa, ambacho wakati mwingine kinafikia hatua ya uchochezi, dhidi ya Watu wa Gaza na Wananchi wa Palestina kwa ujumla, na hata Lebanon ambayo imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi hayo mabaya na yasiyo ya haki.
Huzuni yetu ya kuondokewa na kiongozi wetu, bwana na mtoa ilham wetu, Katibu Mkuu wa Hezbollah, Sayyid Hassan Nasrallah, ni ya kina, na ni kubwa, na haiwezi kuelezeka.
Aliongoza Upinzani (Muqawamah) huu uliobarikiwa na wa ushindi, upinzani ambao ulipata ushindi usio na kifani na kuashiria matukio makubwa ambayo yatabakia milele, na hayo yote ni kwa fadhila ya uongozi wake, hekima yake na ujasiri wake.
Na juu ya yote, hayo yametokana na imani yake, uaminifu na utayari wake wa kukitoa kila kitu katika njia hii bora. Ni njia bora ambayo aliiamini na kuishikilia yeye pamoja na watu wake, Familia yake, Familia za Mashahidi na Majeruhi... .)
Sayyid Safiyyu al-Din alitakiwa kutoa hotuba hii siku hiyo hiyo alipouawa Shahidi katika shambulio la anga la Wazayuni katika eneo la Dahiya, Kusini mwa Beirut.
Maoni yako