dua za kila siku (12)
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya 29
Ee Mwenyezi Mungu! Nifunike katika mwezi huu kwa rehema, Uniruzuku uongofu na kulinda na machafu, Utahirishe moyo wangu usiingiwe na giza la shaka Ewe Mrehemevu wa waja wako walio wema.
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya 28
Ee Mwenyezi Mungu! Niongezee fungu langu la mwezi huu kutokamana na nyongeza, unikirimu katika mwezi huu niyakinishe maombi. Njia zangu za kukufikia ziwe karibu miongoni mwa njia.
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya 27
Ee Mwenyezi Mungu! Niruzuku katika mwezi huu fadhila za usiku wa Laylatul Qadri, Uyageuze mambo yangu yaliyo mazito ili yawe mepesi. Uzikubali nyudhuru zangu, Uniepushe (na Unifutie) madhambi…
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya 25
Ee Mwenyezi Mungu! Nijaalie katika mwezi huu niwe mwenye kuwapenda watu wako (uwapendao) na unijaalie niwe mwenye kutenda Sunna za Mtume wako wa mwisho (Muhammad (s.a.w.)). Ewe Mwenye kuzitakasa…
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya 24
Ee Mwenyezi Mungu! Ninakuomba katika mwezi huu (Unijaalie niyatende) yanayokuridhisha. Na ninajilinda kwako na yanayokuudhi. Na ninakuomba kuniwafikia katika mwezi huu nikutii pasina kukuasi,…
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya 23
Ee Mwenyezi Mungu! Nisafishe katika mwezi huu ili nitokamane na madhambi, Unitakase na aibu (zote) Uuonjeshe moyo wangu Taqwa ya nyoyo (za wanaokuogopa) Ewe Msamehevu wa matelezo ya wenye dhambi.
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya 22
Ee Mwenyezi Mungu! Nifungulie katika mwezi huu milango ya fadhila zako, na Uniteremshie katika mwezi huu baraka zako Uniwafikie katika mwezi huu niyatende yanifikishayo kwenye Radhi yako, Uniweke…
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya ishirini na moja
Ee Mwenyezi Mungu! Nioneshe njia ya kuifikia Radhi yako, wala Usimpe Shetani nafasi ya kunihangaisha katika mwezi huu. Uijaalie Pepo iwe ndiyo mashukio yangu na mapumziko. Ewe Mwenye kuzitekeleza…
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya ishirini
Ee Mwenyezi Mungu! Nifungulie milango ya peponi (ili niingie kwa haraka), na Unifungie milango ya moto (ili nisipate kuingia humo) Uniwafikie kuisoma Qur'ani kwa wingi sana katika mwezi huu,…
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya kumi na tisa
Ee Mwenyezi Mungu! Niongezee fungu langu la baraka za mwezi huu, na Unisahilishie njia ya kuyafikia mema ya mwezi huu, wala Usininyime kukubaliwa mema, Ewe Aongozaye kwenye haki iliyo wazi.
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya kumi na nane
Ee Mwenyezi Mungu! Nizindushe katika mwezi huu ili nipate baraka za masiku yake, Uninawirishe moyo wangu kwa mwangaza wa nuru zake (Nuru za mwezi huu wa Ramadhani) Uvishike viungo vyangu vyote…
-
DiniDua za kila siku za Mwezi wa Ramadhani; siku ya kumi na saba
Ee Mwenyezi Mungu! Niongoze katika mwezi huu kwenye amali njema, Unitekelezee katika mwezi huu haja zangu na mataraji yangu, Ewe Usiyehitaji ufasiri na kuuliza (ndipo ukaifahamu haja ya mja,…