Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Habari la Hawza kutoka mkoani Hormozgan Iran, ujumbe uliotumwa na Baraza Kuu la Hawza, ambao uliundwa na Ayatullah Jawad Marwi, Katibu wa Pili wa baraza hilo, pamoja na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ahmad Farukhfal, Mkuu wa Sekretarieti ya Baraza Kuu; Muhammad Hussein Reza Zadeh, Mkuu wa Ofisi ya Uangalizi na Ukaguzi; Khairullah Salehi, Mkuu wa Ofisi ya Mipango na Utekelezaji; pamoja na wakurugenzi wengine wakuu wa Sekretarieti ya Baraza Kuu, ulitembelea wilaya ya Minab katika safari yake ya mkoani Hormozgan.
Kukutana na wanafunzi wa Hawza, wanazuoni na watu wenye elimu ya juu, pamoja na wanazuoni wa Kishia na Kisunni, na pia kutoa heshima kwa familia za mashahidi wa wilaya hiyo, hususan familia za mashahidi wa Shule ya Shajaratut-Tayyiba, ni miongoni mwa programu zilizotekelezwa na ujumbe wa Baraza Kuu la Hawza katika wilaya ya Minab.
Mkutano wa wanafunzi wa Hawza, walimu na wanazuoni wa wilaya ya Minab
Ayatullah Marwi, Katibu wa Pili wa Baraza, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa wanazuoni na wahubiri wa Hawza ya wilaya ya Minab, alieleza kuhusu nafasi ya wilaya hiyo na kusema: “Nina furaha kubwa kwamba, tukiwa pamoja na ujumbe uliotumwa na Baraza Kuu la Hawza kwenda mkoani Hormozgan, tumefanikiwa kufika katika mji wa Minab; mji wa Muqawama na wa kudhulumiwa, mji wa nguvu na ushujaa, na kushiriki katika mkutano huu mbele ya wanazuoni, walimu, wanafunzi wa Hawza na watafiti.”
Alisisitiza kuwa: “Baada ya vita vya siku 12 na siku 40, pamoja na kuuawa shahidi Kiongozi Mkuu aliyeuawa kishahidi, jukumu la wanazuoni wa dini limekuwa zito sana, wanapaswa kuendeleza jihadi tatu kwa wakati mmoja.”
Kwanza: Jihadi dhidi ya adui wa Marekani na Uzayuni
Katibu wa Pili wa Baraza Kuu la Hawza alitaja uwepo endelevu wa wanazuoni wa dini katika medani ya jihadi dhidi ya adui wa Marekani na Uzayuni kuwa jukumu la kwanza la wanazuoni hao, alisema: “Uwepo wa wanazuoni wa dini katika medani ya jihadi ni jambo muhimu sana, kama ambavyo katika kipindi cha miaka minane ya Vita vya Kujihami Vitakatifu, wanazuoni na watu mashuhuri miongoni mwa wanazuoni wa dini walikuwa na uwepo endelevu katika medani za mapambano.”
Akieleza kuwa hata leo kuambatana na wapiganaji na mashujaa wanaopambana bado ni jukumu muhimu zaidi la wanazuoni wa dini.
Aliongeza kwa kusema: “Katika kipindi cha miaka minane ya Vita vya Kujihami Vitakatifu, wanazuoni na watu mashuhuri miongoni mwao walifika katika mstari wa mbele wa jihadi na kuwa pamoja na wapiganaji. Kwa mfano, Ayatullah Meshkini, Ayatullah Sadduqi, Ayatullah Ashrafi Isfahani, na hata Marji' wa Taqlidi kama Ayatullah al-Udhma Wahid Khorasani pamoja na Maraji' wengine wa Taqlidi, kwa kuwepo katika medani za mapambano ya haki dhidi ya batili, walikuwa nguzo imara ya kuwaunga mkono wapiganaji na kuwapa moyo.”
Pili: Jihadi ya kielimu: Mwalimu mashuhuri wa Hawza ya Qum, katika kuendelea na maelezo yake, aligusia kuongezeka wimbi la watu duniani wanaoielekea na kuyapa kipaumbele mafundisho ya Ahlul-Bayt (as), kisha akasema: “Leo hii, watu katika maeneo mbalimbali ya dunia wanatafuta misingi na mafundisho ya Mapinduzi ya Kiislamu. Kwa hiyo, wanafunzi wa Hawza wanapaswa kusoma ili kukidhi hitaji hili, wala si kwa ajili ya Minab, mji wao au kitongoji chao pekee.”
Tatu, Jihadi dhidi ya nafsi: Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, alilitaja jukumu la tatu la wanazuoni wa dini, sambamba na jihadi ya kujihami na jihadi ya kielimu, kuwa ni jihadi dhidi ya nafsi. Alisema: “Watu wenye elimu na uwezo mkubwa miongoni mwa vijana wa Hawza hawapaswi kupuuza jihadi hii kubwa zaidi.”
Katika mkutano huo, baadhi ya wanazuoni, walimu na wanafunzi wa Hawza walitoa hotuba na kueleza changamoto pamoja na maswali yao. Ayatullah Marwi naye aliwajibu maswali yao.

Hafla ya kuwakumbuka mashahidi wa Shule ya Shajaratut-Tayyiba
Katika kuendelea na programu za ujumbe wa Baraza Kuu la Hawza katika wilaya ya Minab, ilifanyika hafla ya kuwakumbuka mashahidi wa Shule ya Shajaratut-Tayyiba na kutoa heshima kwa familia tukufu za mashahidi hao.
Katika hafla hiyo, Ayatullah Marwi aliwasilisha salamu na rambirambi za Maraji' wa Taqlidi na walimu wa Hawza kwa familia zilizofiwa, huku akisisitiza umuhimu na nafasi ya tukio hilo katika historia ya zama za hivi karibuni.
Akizungumzia umuhimu wa kuitambulisha kwa ulimwengu jinai ya adui wa Marekani na Uzayuni katika shambulio dhidi ya Shule ya Minab, alisema: “Kuelewa kwa kina uchungu na mateso wanayopitia familia zilizofiwa kunatuchochea kuchukua hatua. Kama ambavyo Bibi Zainab (as), baada ya tukio la Karbala, aliufikisha ujumbe wa Ashura kwa watu duniani kote, vivyo hivyo, leo hii viongozi na wote wenye dhamana wanapaswa kutimiza wajibu wao wa tukio la Shule ya Shajaratut-Tayyiba, kwa kuhifadhi kumbukumbu za kujitolea huku kukubwa na kulitambulisha tukio hili kwa ulimwengu.”
Mjumbe huyo wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, akiwahutubia wazazi na familia za mashahidi wa tukio hilo, alieleza kuwa jukumu lao linazidi kuwa zaidi ya kuomboleza tu, na kuongeza: “Damu iliyomwagika imebeba jukumu zito. Ninyi ni mifano mikubwa kwa jamii za wanadamu, na mnapaswa kujiandaa kutangaza ujumbe wa jukumu hili, lengo letu la kufika hapa si kutoa hotuba tu, bali ni kujifunza kutokana na kujitolea huku kukubwa.”
Aidha, akigusia nguvu na mamlaka ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kauli za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Mungu azidi kumhifadhi), alisisitiza: “Adui anajaribu, kwa kuanzisha matukio mbalimbali, kuwatenganisha watu na Mapinduzi ya Kiislamu. Hata hivyo, Jamhuri ya Kiislamu imesimama imara mbele ya adui kwa nguvu na mamlaka yake. Kama ambavyo Kiongozi Mkuu amesisitiza kulipiza kisasi dhidi ya adui, nasi pia tumeazimia kuendelea katika njia ya kuhifadhi tunu za Mapinduzi na kuunga mkono Muqawama.”
Maoni yako