Jumapili 1 Novemba 2026 - 23:45
Mustakabali wa Watawala wa Nchi Ndogo Ndogo za Ghuba ni wa Giza

Naibu Katibu wa Pili wa Baraza Kuu la Hawza nchini humo amesema kuwa; hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya mwanazuoni mpambanaji, Ustadh Sheikh Hussein Al-Matouq, pamoja na kundi la Mashia, inatokana na kukata tamaa watawala wa nchi ndogo ndogo za eneo la Ghuba ya Uajemi katika kukabiliana na wananchi na wasomi wao.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawad Marwi, mwanzoni mwa darsa yake ya juu ya fiqhi, amelaani vikali hukumu zisizo na huruma zinazotolewa na mahakama za eneo hilo dhidi ya wananchi, vijana na wanazuoni mashuhuri, hususan hukumu ya dhuluma iliyotolewa na watawala wa Kuwait ya kumuua mwanazuoni mpambanaji, Ustadh Sheikh Hussein Al-Matouq, pamoja na kundi la Mashia.

Naibu Katibu wa Pili wa Baraza Kuu la Hawza nchini Iran, amesema kuhusiana na suala hilo kuwa: "Hukumu ya kifo dhidi ya mwanazuoni mpambanaji, Ustadh Sheikh Hussein Al-Matouq, pamoja na kundi la Mashia, inatokana na kukata tamaa watawala wa nchi ndogo ndogo za eneo la Ghuba ya Uajemi katika kukabiliana na wananchi na wasomi wao."

Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum amesisitiza kuwa; kukamatwa, kuteswa na kutolewa hukumu za kifo na mfumo wa mahakama wa watawala hao wanaotegemea Marekani na utawala wa Kizayuni ni matokeo ya mkwamo waliojitia wenyewe watawala hao, ambao hautazaa matunda mengine isipokuwa kuzidi kuzama ndani yake.

Kwa mujibu wa Ayatullah Marwi, ni wanazuoni hao, wasomi na Mashia wanaodhulumiwa wa Kuwait ambao walisimama kidete dhidi ya uvamizi wa Saddam wa Kibaathi.

Mwalimu wa masomo ya juu katika Hawza ya Qum, amesisitiza jambo hili muhimu akieleza kuwa; hatua za aina hii zisizo na busara zitasababisha wananchi wa eneo hilo kuzidi kupata mwamko, huku zikizidisha hali ya kutokuwa na uwezo kwa watawala wa nchi hizo ndogo ndogo, ameongezea kuwa mustakabali wa watawala hao ni wa giza.

Naibu Katibu wa Pili wa Baraza Kuu la Hawza nchini Iran, amelaani vikali hatua hizo na kusema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua itakazoona zinafaa na zenye maslahi."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha