Jumanne 20 Oktoba 2026 - 13:00
Ombi la Kujiuzulu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Baada ya Maandamano ya Wananchi

Hawza/ Kufuatia maandamano ya wananchi nchini Ufaransa, serikali ya nchi hiyo inakabiliwa na shinikizo linalozidi kuongezeka. Ombi la kutaka Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu pamoja na ukosoaji wa mkakati wa serikali wa kudumisha utulivu na usalama wa umma vimeathiri hali ya kisiasa nchini humo.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, maandamano makubwa ya wanafunzi na wananchi yaliyofanyika nchini Ufaransa yameisababishia serikali ya nchi hiyo kukabiliwa na wimbi la shinikizo la kisiasa na ukosoaji. Katika mazingira ambayo wito wa kutaka Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu unazidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha habari cha France 24, siku ya Jumapili, tarehe 18 Oktoba, serikali ya Ufaransa ilikabiliwa na shinikizo kubwa kufuatia maandamano yaliyotokea pembezoni mwa maandamano mengine yaliyokuwa yakiendelea nchini humo. Wito wa kutaka Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu, pamoja na ukosoaji dhidi ya mkakati wa serikali katika kudumisha utulivu na usalama wa umma, umeongeza shinikizo dhidi ya serikali kuu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha