Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 19 za Kiarabu na Kiislamu wamepinga uamuzi wa Colombia wa kufungua ubalozi Jerusalem, na kuitaka serikali ya nchi hiyo kuupitia upya uamuzi huo na kuufuta.
Colombia ilifungua ubalozi wake mjini Jerusalem katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Colombia, Rosa Yolanda Villavicencio Mapy, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Sa’ar.
Katika taarifa yao ya pamoja, mawaziri hao wa mambo ya nje walisema kuwa hatua hiyo inakiuka maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kudhoofisha juhudi za kimataifa zinazolenga kufikia amani ya haki na ya kudumu.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa hatua au uamuzi wowote unaolenga kubadilisha hadhi ya kisheria au ya kihistoria ya Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu, au kuutambua kuwa mji mkuu wa Israel, ni batili na hauna uhalali wowote wa kisheria.
Mawaziri hao wa mambo ya nje walirejelea Maazimio Na. 476 na 478 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, yaliyopitishwa mwaka 1980. Maazimio hayo yanapinga mabadiliko katika hadhi na utambulisho wa Jerusalem, na kuzitaka nchi mbalimbali kuondoa uwakilishi wao wa kidiplomasia kutoka katika mji huo.
Chanzo: pajhwok.com
Maoni yako