Alhamisi 17 Septemba 2026 - 03:00
Waislamu ni nguvu inayochipuka mjini New York

Hawza/ Waislamu ni nguvu inayochipuka mjini New York, na Palestina ina umuhimu mkubwa kwao; jambo ambalo linachukuliwa kuwa kengele ya tahadhari kwa matajiri na Wazayuni.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, baadhi ya watu wanafanya juhudi kubwa za kuwatambulisha Waislamu kuwa ni maadui wakuu wa maendeleo ya New York. Hata hivyo, kwa sasa Waislamu wa jiji hilo wanajitahidi kuchora mustakabali wa baadaye kupitia uelimishaji kuhusu Uislamu.

Kundi la watu wenye misimamo mikali, ambao wanawachukulia Waislamu na Uislamu kuwa ndio waliohusika na tukio la Septemba 11, lilipinga uwepo wa Mwislamu yeyote katika kumbukumbu ya tukio hilo. Hata hivyo, Waislamu wa New York walihudhuria tena mkusanyiko huo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi na uelewa, huku wakitoa pole kwa familia za waliofariki. Miongoni mwa waliopoteza maisha katika tukio hilo walikuwapo pia Waislamu waliojitolea, akiwemo daktari mmoja Mwislamu wa Marekani.

Gazeti la The Guardian limechambua kwamba Waislamu ni nguvu inayochipuka mjini New York na kwamba Palestina ina umuhimu mkubwa kwao; jambo ambalo linachukuliwa kuwa kengele ya tahadhari kwa matajiri na Wazayuni.

Watu wenye misimamo mikali mjini New York pamoja na mabepari Wayahudi wanadai kwamba Mamdani na Abdul El-Sayed, mgombea wa chama cha Kidemokrasia wa Seneti huko Michigan, wanakataa kutoa utiifu wa mara kwa mara kwa utukufu wa Marekani, na wanathubutu kuzungumzia suala la kuungwa mkono kwa Israel na Marekani, pamoja na madhara mabaya ya “vita dhidi ya ugaidi” katika Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, licha ya shinikizo hizo, Waislamu wa New York, pamoja na kuwepo kwa makundi mbalimbali miongoni mwao—wakiwemo wanaoamini dini na wasiokuwa waumini wanaouona Uislamu kama utamaduni pekee—wanajitahidi kuwa na umoja na kutoa uelewa kuhusu Uislamu. Hivi karibuni, mtazamo ambao umeenea sana katika mijadala ya New York umeibuka kwa kauli kwamba hivi karibuni kizazi kipya, kinachoitwa kizazi cha “SWANA” — yaani Asia ya Kusini-Magharibi na Afrika Kaskazini, eneo linalojumuisha nchi kuanzia Palestina hadi Iran na Sudan — kitafikia madaraka nchini Marekani na mjini New York. Mtazamo na madai haya yamesababisha mijadala na mabishano mengi nchini humo.

Chanzo: Imenukuliwa kutoka katika ripoti ya The Guardian.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha