Jumanne 15 Septemba 2026 - 10:18
Kukombolewa pwani ya magharibi ya Yemen ni kofi kubwa kwa miradi ya Kizayuni na Marekani

Hawzah/ Vikosi vya Hizbullah Iraq, vimeelezea kuwa ushindi wa kimkakati wa Vikosi vya Wanajeshi na watu huru wa Yemen katika mapambano ya kuwasafisha wavamizi katika maeneo ya pwani ya magharibi mwa nchi hiyo ni kofi kubwa kwa miradi ya Kizayuni na Marekani, huku vikiwapongeza wananchi wa Yemen pamoja na mashujaa wa Vikosi vya Wanajeshi na Ansarullah.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama la Shirika la Habari la Hawza, Vikosi vya Hizbullah Iraq vimewapongeza wananchi wa Yemen pamoja na mashujaa wa Vikosi vya Wanajeshi na Ansarullah kwa ushindi huo mkubwa wa kimkakati, uliopatikana kupitia mapambano ya kusafisha maeneo ya pwani ya magharibi, kusini-magharibi mwa Yemen, na kuwafukuza vibaraka wa wavamizi pamoja na mamluki wao.

Katika taarifa rasmi ya Hizbullah Iraq iliyotolewa kufuatia maendeleo ya hivi karibuni ya uwanja wa vita, Vikosi vya Hizbullah viliwasilisha pongezi na salamu za juu kabisa kwa wananchi wa Yemen na mashujaa wa Vikosi vya Wanajeshi na Ansarullah, kwa ajili ya mafanikio hayo makubwa katika njia ya kurejesha kikamilifu mamlaka ya kitaifa ya Yemen huru na kuitakasa ardhi yake kutokana na uchafu wa utawala wa kibeberu wa Saudi Arabia unaotawaliwa na vibaraka, huku vikisifu mafanikio hayo.

Vikosi vya Hizbullah vilisisitiza: Mafanikio haya ya uwanja wa vita ni kofi kubwa kwa miradi ya adui Mzayuni na Marekani pamoja na vibaraka wao katika eneo hilo, na ni hasara kubwa kwa utawala wa kihalifu wa Saudi Arabia unaoongozwa na Muhammad bin Salman, ambao umetumia makumi ya mabilioni ya dola katika juhudi za kuilazimisha Yemen pendwa ipige magoti.

Taarifa hiyo ilisisitiza: Ushindi huu usingeweza kupatikana isipokuwa kwa imani thabiti, kumtegemea kikamilifu Mwenyezi Mungu na kushikamana na madhehebu ya Ahlul-Bayt watukufu (as), sambamba na ustahimilivu wa kishujaa na kujitolea kwa kiasi kikubwa kwa watu huru wa Yemen katika miaka yote ya mapambano magumu ya kukomesha enzi ya kijeshi na uvamizi wa kigeni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha