Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Vikosi vya Mapinduzi ya Bahrain, katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya kufanyika kikao cha mara kwa mara cha wawakilishi wao kwa ajili ya kujadili maendeleo ya hivi karibuni nchini humo, vimelaani mashauri yasiyo ya haki dhidi ya maulama wakubwa wa dini na tuhuma za kubuniwa wanazotuhumiwa nazo. Tuhuma hizo zinawekwa katika mfumo wa kulengwa kwa utaratibu, jambo linaloonesha kwamba serikali, hasa baada ya vita vys kulazimishwa dhidi ya Iran, imeelekea katika viwango vya hatari.
Serikali imeamua kuanzisha vita vya kuwaondosha watu na mateso, na imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha kutishia uwepo wa wenyeji wa asili, utambulisho na matakatifu ya watu wa Bahrain. Kesi zinazowakabili maulama wakubwa wa dini ni ishara ya vita vya wazi dhidi ya haki, itikadi na wananchi. Kadiri serikali inavyosisitiza kuendelea na kesi hii ya kuchekesha na hukumu za dhuluma ambazo huenda zikatolewa kutokana nayo, ndivyo jukumu lake litakavyokuwa kubwa zaidi, na itawajibika kwa madhara yote yatakayotokana na hatua hizo.
Hisia za jazba na hotuba za uchochezi zinazoambatana na vikao vya kesi za maulama zinalaaniwa vikali. Aidha, imeelezwa kwamba mazingira yanayolindwa na serikali, kwa sura na maudhui yake, kwa hakika ni kesi dhidi ya uwepo wa Mashia nchini Bahrain. Kwa hiyo, wadau wote wameombwa kujihadhari na madhara mabaya yatakayotokana na kuingizwa katika njia hii ya kichaa, ambayo inatishia usalama na utulivu wa nchi.
Maulama wakubwa wa dini daima wataendelea kuwa alama angavu ya heshima na utu, walinzi wa dini na chanzo cha fahari ya taifa. Dhuluma na kifungo havitaweza kupunguza hata chembe hadhi yao ya juu wala historia yao yenye kung'aa. Serikali inapaswa kukata tamaa mara kwa mara katika juhudi zake za kuwatenganisha wananchi waaminifu na maulama pamoja na alama zao, kwa sababu wananchi wataendelea kuinua vichwa vyao kwa fahari kutokana na vilemba hivi na taji hizi zenye kung'aa.
Mwisho wa taarifa hiyo wameeleza: Harakati za wananchi za kufikia malengo yao halali ya kisiasa katika nyanja za uhuru na haki zitaendelea, hata kama ugaidi na mzingiro wa serikali vitaongezeka, na hata kama changamoto katika eneo zitaongezeka na nguvu za wavamizi zitaungana, wananchi wa Bahrain hawatapiga magoti, hawatasalimu amri wala hawatarudi nyuma. Bendera ya wananchi hawa itaendelea kuinuliwa kwa azma yenye nguvu zaidi na utukufu usio na mipaka, na siku zitaonesha kushindwa kwa chaguzi zote za ukandamizaji, mateso na utegemezi kwa mataifa ya nje.
Maoni yako