Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Yasin Mousavi, Imam wa Ijumaa wa Baghdad na mwanazuoni mashuhuri wa Hawza ya Najaf Ashraf, akizungumzia mjadala ulioibuka katika wiki za hivi karibuni kuhusu suala linaloitwa “kuhodhi silaha mikononi mwa Serikali”, alisema: Mijadala hii imeambatana na mkanganyiko na vurugu kubwa katika uwanja wa kisiasa na wa vyombo vya habari. Alionya kuhusu jitihada za kufafanua dhana ya “silaha ya Serikali” kwa kuzingatia mtazamo wa Marekani au ajenda za kisiasa zinazolenga kuidhoofisha Iraq.
Ayatullah Mousavi katika khutba za Swala ya Ijumaa mjini Baghdad alisisitiza: Kupinga “silaha zisizo na udhibiti na zilizo nje ya mamlaka ya Serikali” ni jambo la hakika na lisilobadilika, na Marja’iyyah ya kidini pia imesisitiza mara kadhaa umuhimu wa kuweka silaha kwenye kuihudumia Serikali; lakini suala kuu ni kufafanua silaha halali, si majina na vyeo.
Aliongeza: Marja’iyyah tukufu imekuwa na msimamo wa wazi wa kutaka silaha zipangwe na kudhibitiwa, na uzoefu wa Iraq pia umethibitisha hatari za silaha zilizo nje ya mfumo wa sheria; hata hivyo, baadhi ya pande zinajaribu kuzuia dhana ya “silaha ya Serikali” kwa jeshi, polisi na baadhi ya taasisi rasmi pekee. Imam wa Ijumaa wa Baghdad alifafanua kuwa: “Suala si jina wala cheo, bali ni ukweli na kazi ya silaha katika kuilinda Serikali na nchi.”
Kuanguka kwa Mosul; Mtihani wa Kufafanua “Silaha ya Serikali”
Ayatullah Mousavi, akirejea matukio ya kuanguka kwa Mosul mwaka 2014, alilitaja tukio hilo kuwa mfano unaoonesha kwamba; kuwa na hadhi ya taasisi ya kijeshi pekee hakutoshi kuhakikisha ulinzi wa nchi. Alisema: Vikosi vinne vya kijeshi vilisambaratika ndani ya saa chache na silaha za kisasa pamoja na kiasi kikubwa cha mali zao wakakiachia kikundi cha kigaidi cha Daesh; kwa upande mwingine, walijitolea walioingia uwanjani kufuatia fatwa ya Marja’iyyah kuhusu jihadi ya lazima kwa pamoja (jihad al-kifayah), kutokana na uhaba wa vifaa vya kijeshi wakati huo, walitegemea msaada wa wananchi wa Iraq katika kupata chakula na mahitaji ya kuwawezesha kuendelea na mapambano.
Ayatullah Mousavi aliongeza: “Ilikuwa ni mawakibu za Imam Hussein (as) zilizochukua jukumu la kutoa chakula kwa mamia ya maelfu ya wajitolea, wakati ambapo kambi za kijeshi zilikuwa zikikabiliwa na uhaba wa silaha na mafunzo.”
Alisisitiza kuwa: Al-Hashd al-Sha’bi ni sehemu ya silaha ya Serikali ya Iraq; kwa sababu waliingia katika uwanja wa mapambano kwa kuitikia fatwa ya Marja’iyyah na kwa ajili ya kuilinda Iraq. Aliongeza kwamba; uhalali unapaswa kupimwa kwa kuzingatia uhusiano halisi na Serikali na kulinda nchi, si kwa kutegemea tu majina na miundo ya kiutawala.
Imam wa Ijumaa wa Baghdad alisema: “Al-Hashd ni silaha ya Serikali, na silaha ya Muqawama pia ni ile silaha iliyokuwa na nafasi katika kuondoka kwa vikosi vya Marekani kutoka Iraq; na hili ni jambo ambalo hata Wamarekani wenyewe wamelikiri.”
Kukosoa Utegemezi wa Jeshi la Iraq kwa Marekani Katika Silaha
Ayatullah Mousavi aliendelea kwa kumtaka Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iraq kutafuta vyanzo mbalimbali vya silaha kwa ajili ya kuimarisha jeshi la nchi hiyo na kuliondoa katika utegemezi wa silaha kutoka Marekani.
Alisema: “Ikiwa mnataka kurekebisha taasisi ya kijeshi, lazima mnunue ndege na silaha nzito kutoka nchi nyingine na kujenga upya uwezo wa jeshi; kwa namna ambayo mtahakikisha uhuru wa maamuzi ya Iraq.”
Imam wa Ijumaa wa Baghdad pia alimkosoa vikali Donald Trump, Rais wa Marekani, na Tom Barrack, mjumbe wa Marekani, na akasema kuiwekea Iraq mwisho kuhusu silaha za makundi ya Muqawama kuwa ni uingiliaji usiokubalika katika mambo ya ndani ya nchi hiyo.
Alisisitiza: “Hakuna nguvu yoyote ya kigeni yenye haki ya kuingilia maamuzi ya mamlaka ya Iraq”, na akakosoa jitihada za Washington za kuilazimisha Serikali ya Iraq kukubali mtazamo wake.
Ayatullah Sayyid Yasin Mousavi alihitimisha hotuba yake kwa kusema: Ikiwa Marekani haitakubali masharti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, italazimika kuondoka katika eneo hili. Aliongeza: Iran imeingia katika hatua ya “kuamua hatima kwa njia ya kijeshi”, na vikosi vya Iran vina uwezo wa kuviondoa vikosi vya Marekani katika eneo hilo.
Maoni yako