Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Islamic Analysis, Bunge la Jordan, wakati wa kujadili pendekezo la kutuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kuuawa kwa wanajeshi wa Marekani katika shambulio lililolenga kambi ya kijeshi ndani ya ardhi ya nchi hiyo, lilishuhudia mabishano na tofauti za maoni kati ya wabunge.
Ali Al-Hulayleh, mbunge wa Jordan, katika kikao cha Jumapili alipendekeza kuwa Bunge la nchi hiyo litume rasmi ujumbe wa rambirambi kwa Bunge la Marekani kufuatia kuuawa kwa wanajeshi wa Marekani. Hata hivyo, kutokana na msimamo wa Washington kuhusu vita vya Ghaza, pendekezo hilo lilisababisha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wabunge.
Upinzani mkubwa kutoka kwa wabunge
Wabunge waliopinga pendekezo hilo walieleza kwamba, kutokana na uungaji mkono wa kisiasa na kijeshi wa serikali ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni katika operesheni zake za kijeshi dhidi ya Ukanda wa Ghaza, kutuma ujumbe wa rambirambi kwa Marekani katika mazingira hayo hakukubaliki.
Pia walieleza kuwa, kutokana na kuongezeka kwa hasira na kutoridhika kwa maoni ya umma nchini Jordan dhidi ya sera za Washington, hatua kama hiyo ingekuwa kinyume wazi na hisia pamoja na msimamo wa jamii ya Jordan.
Taifa la Jordan ni kubwa kuliko kutuma ujumbe wa aina hiyo wa rambirambi
Wabunge waliopinga pendekezo hilo, wakifafanua sababu za msimamo wao na wakirejelea hali ya kisiasa ya nchi pamoja na uungaji mkono wa wananchi wa Jordan kwenye kadhia ya Palestina, walisema: "Marekani ndiye msaidizi mkubwa zaidi wa operesheni za kijeshi na mauaji yanayoendelea Ghaza. Kwa kuzingatia hasira za maoni ya umma dhidi ya Washington, hadhi, msimamo na dhamiri ya taifa la Jordan ni ya juu zaidi kuliko kutuma ujumbe wa rambirambi kwa Marekani."
Mwitikio mkubwa katika mitandao ya kijamii
Tofauti hiyo ya maoni, ambayo ilianza ndani ya ukumbi wa Bunge, ilisambaa kwa haraka pia katika mitandao ya kijamii. Pendekezo la Ali Al-Hulayleh, ambalo lilitolewa kwa kuzingatia uhusiano wa jadi kati ya Amman na Washington, liliungwa mkono na idadi ndogo tu ya wabunge. Aidha, katika mitandao ya kijamii lilikabiliwa na wimbi kubwa la ukosoaji, hali ambayo inaashiria kuongezeka kwa hisia za kuipinga Marekani miongoni mwa jamii ya Jordan.
Maoni yako