Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza mjini Kashan, Salim al-Muslimawi, mwakilishi wa Bunge la Iraq na gavana wa zamani wa Hilla, katika mkutano wake na Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qamsar, mji mkuu wa maua na maji ya waridi wa Iran, pamoja na kundi la maulamaa, wenye viwanda na viongozi wa kaunti za Kashan na Aran wa Bidgol, alisema: Kwangu mimi ni heshima na fahari kubwa kuwa mwenyeji wa ujumbe huu mtukufu na wenye wasomi kutoka wilaya ya Kashan ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mwakilishi wa Bunge la Iraq, akilihutubia kundi la wageni kutoka eneo la Kashan lililofika kwenye Ataba Tukufu, alisisitiza: Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu nyinyi wapendwa nchini Iraq, katika ardhi takatifu ya Najaf Ashraf na Karbala Mualla.
Gavana wa zamani wa Hilla, akieleza kwamba Iraq na Iran ni mataifa mawili ya kidugu yenye mizizi ya pamoja katika itikadi za Kiislamu, maadili ya kidini na mipaka ya kijiografia, alisema: Ukaribu wa kitamaduni na kufanana kwa desturi na mila zetu umeunda uhusiano wa kina wa moyoni kati ya taifa la Iraq na taifa la Iran.
Salim al-Muslimawi alieleza kwamba; umoja na mshikamano wa watu wa nchi mbili za Iran na Iraq ni alama wazi ya umoja wa ulimwengu wa Kiislamu na chanzo cha heshima na nguvu ya Umma wa Kiislamu, na akasema: Ninasisitiza umuhimu wa kuendelezwa na kupanuliwa kwa ushirikiano wa pande hizi mbili, hususan katika nyanja za kidini, kitamaduni na kielimu. Aidha, ushirikiano huu utakuwa dhamana ya kuhifadhi utambulisho wa Kiislamu na kuimarisha nafasi ya mataifa haya mawili katika eneo hili.
Mwakilishi wa Bunge la Iraq mwishoni alisisitiza kwa kusema: Ninatoa shukrani na pongezi zangu kwa juhudi zenu za dhati katika nyanja za kidini na katika kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s.), na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajalie mafanikio zaidi na zaidi.
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qamsar pia, huku akitoa shukrani kwa mapokezi mazuri sana yaliyotolewa na viongozi wa Iraq kwenye msafara wa kitamaduni wa wapenzi wa Uimamu na Wilaya kutoka eneo la Kashan ndani ya Ataba Tukufu, alielekeza kwenye uwezo mkubwa wa kidini na kimadhehebu wa eneo la Kashan na kusisitiza juu ya kupanuliwa kwa mahusiano ya kibiashara, kiuchumi, kitalii, kitamaduni na kidini kati ya nchi mbili za Iran na Iraq.
Mwanzoni mwa mkutano huu pia, viongozi wa wilaya za Kashan na Aran wa Bidgol walieleza uwezo wa kitamaduni, kihistoria na wa ziara za kidini za eneo la Kashan na kusisitiza juu ya kuimarishwa kwa mahusiano ya kitamaduni, ya ziara za kidini na kibiashara kati ya nchi mbili za Iran na Iraq.
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qamsar, mwakilishi wa Ofisi ya Gavana wa Kashan, wawakilishi wa Ataba Tukufu za Ali bin Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) huko Ardehal na Muhammad Hilal bin Ali (a.s.) wa wilaya ya Aran wa Bidgol, wajumbe wa Baraza la Kiislamu la Jiji la Kashan, mwakilishi wa Manispaa ya Kashan pamoja na menejimenti ya Kampuni ya Kusokota, na Kufuma Nguo ya Kashan, pi walihudhuria mkutano huu.
Maoni yako