Jumatatu 25 Mei 2026 - 12:30
Damu ya watoto wa Minab ni jeraha linalovuja damu moyoni mwa Umma/ Tunaahidi kutonyamaza

Hawza/ Sheikh Ahmad Haidari, mwakilishi wa Majma‘ Al-Alami Qadimun katika mkoa wa Hormozgan, amesema kwamba; damu ya watoto wa Minab ni jeraha linalovuja damu ndani ya moyo wa Umma wa Kiislamu, alisisitiza kwa kusema: “Tunatoa ahadi kwamba hatutanyamaza na hatutaruhusu damu hizi zipotee bure.”

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, katika kipindi cha televisheni “Mashahidi Watoto wa Minab, Sauti ya Madhlumiyyah ya Umma” kilichorushwa Jumamosi tarehe 2 Khordad 1405 (23 May 2026) kwa juhudi za Majma‘ Al-Alami Qadimun kupitia kituo cha Al-Kawthar, Sheikh Ahmad Haidari, mwakilishi wa majma hiyo katika mkoa wa Hormozgan, alieleza vipengele mbalimbali vya janga la shule ya Minab na wajibu wa Umma wa Kiislamu mbele ya jinai hiyo.

Sheikh Ahmad Haidari, akisisitiza kwamba; janga hili halijawahi kushuhudiwa katika historia ya Uislamu, alisema: “Jambo hili halikutokea katika zama za Mtume Mtukufu (saww), wala katika enzi za Maswahaba, wala katika karne zilizofuata, janga hili limetokea siku chache zilizopita tu, na mzigo wake hauko juu ya Iran pekee, bali juu ya Umma wote wa Kiislamu, watoto wasio na hatia na wasio na kosa lolote waliuawa kishahidi katika shule ya Minab.”

Akirejelea tofauti kati ya madai na uhalisia, aliongeza: “Hapo awali watu walikuwa wakizungumzia yale yanayotokea Ghaza, kwamba utawala wa Kizayuni unataka kuiteka Ghaza na kuleta amani na ubinadamu nchini Palestina, lakini kile tunachokiona na kukisikia ni kinyume kabisa na madai hayo, kile ambacho utawala wa Kizayuni unakitaka ni kuutawala ulimwengu, si ubinadamu wala amani.”

Mwakilishi wa Majma‘ Al-Alami Qadimun huko Hormozgan aliwaambia watu huru duniani: “Damu ya watoto wetu wa Minab si simulizi la kupita, damu hii ni jeraha linalovuja damu ndani ya moyo wa Umma, hatutarajii uadilifu kutoka kwa wale ambao wao wenyewe hutengeneza mauti, mkono wa Marekani unaoitwa ‘Shetani Mkuu’, ndio unaowalisha wauaji silaha na kuwapatia kinga kwa kila jinai wanayoifanya, vilevile, utawala wa Kizayuni unaoua watoto, ambao hauelewi isipokuwa lugha ya damu, unatumia aina mbaya zaidi za ugaidi dhidi ya usafi na kutokuwa na hatia kwa watoto.”

Kwa hisia kali aliuelekea Umma wa Kiislamu na kusema: “Ewe Umma wa Uislamu! Watoto wetu mashahidi wa Minab si wahanga tu; wao ni sauti ya madhlumiyyah, wanapaza sauti ndani ya dhamiri zetu wakisema: Ghera yenu iko wapi? Ubinadamu wenu uko wapi? Je, tumeridhia kuwa watazamaji wa kuchinjwa kwa watoto hawa wasio na hatia?”

Sheikh Ahmad Haidari alisisitiza: “Damu ya watoto hawa itaamsha dhamiri ya Umma kutoka katika usingizi wa ghafla, hebu tupaze sauti zetu tukisema: ‘Hapana Marekani, hapana utawala wa Kizayuni muuaji.’ Tunawaahidi ninyi watoto kwamba hatutanyamaza, hatutaridhia, na hatutaruhusu damu yenu ipotee bure.”

Akielezea mandhari za kusikitisha za Minab, aliongeza: “Machozi ya mama yanamwagika kwa wingi, machozi haya hayapotei bure; bali ni ahadi iliyo juu ya mabega yetu na wasia ambao haupaswi kupotea katika kelele za dunia, mama anapomlilia mtoto wake, mbingu yote husikiliza, na malaika huandika katika daftari la kumbukumbu kwamba bado katika ardhi hii kuna nyoyo zinazopambana na ukatili, tunawezaje kunyamaza mbele ya maumivu yenye kina hiki na mbele ya kutokuwa na hatia kulikofutwa kabla hata ndoto zake hazijakomaa?”

Mwakilishi wa Majma‘ Al-Alami Qadimun ndani ya mkoa wa Hormozgan, akielezea nafasi ya watoto, alisema: “Utoto si kipindi cha mpito tu katika maisha ya mwanadamu, utoto ni haki ya kwanza, nuru ya kwanza na nyumba ambayo ndani yake roho hujengwa, mtoto asiye na hatia anapopotea ulimwengu haupotezi tu mtoto mmoja na maisha madogo, bali hupoteza sehemu ya ubinadamu wake, kwa hiyo, kuwatetea watoto si msimamo wa muda wa kihisia tu, bali ni mizani ya maadili, kipimo cha ustaarabu na ishara ya ukweli wa kila dai linalozungumzia rehema.”

Alisisitiza kuwa: “Dhulma haidumu milele hata ikiwa itaonekana kuishi muda mrefu, kupaza sauti ya haki huangaza njia, hata kama itachelewa, hatutaki makelele matupu; tunataka mwamko wa dhamiri, heshima ya msimamo na msaada wa kweli kwa wale ambao katika dunia hii hawana chochote isipokuwa nyoyo ndogo na macho yanayong’aa kwa hofu, mwenye uwezo wa kusema, na aseme, mwenye uwezo wa kuonesha mshikamano na afanye hivyo, mwenye uwezo wa kumsaidia aliyedhulumiwa, basi asimame pamoja nasi bila kusita.”

Sheikh Ahmad Haidari, akirejelea athari za kisaikolojia za jinai hii katika kumbukumbu ya pamoja ya Umma, alisema: “Majeraha yanayowapata watoto hayabaki katika miili yao pekee, bali huingia katika kumbukumbu ya Umma na kuwa swali lisilo na jibu ndani ya dhamiri ya historia: ‘Maumivu yalipokuita, ulifanya nini?’ Hili ni swali ambalo lazima tujiulize, je, nyoyo zetu zinafahamu na zimeamka au la?”

Mwishoni mwa hotuba yake, huku akiomba dua na kusisitiza umuhimu wa muqawama wa kiraia wenye heshima, alisema: “Mataifa makubwa hayatambuliwi kwa wingi wa silaha zao, bali kwa ukubwa wa rehema zao na uwezo wao wa kuwalinda wanyonge, ushahidi si alama ya heshima kwa wale tu waliotangulia mbele ya haki, bali pia ni jukumu juu ya mabega ya waliobaki ili wahifadhi kumbukumbu, watimize ahadi na wakatae kusahau.

Hebu tuinue mikono yetu kuelekea mbinguni, si kwa ajili ya kulipiza kisasi, bali kwa ajili ya uadilifu, utulivu na subira njema, tujenge kutoka katika huzuni nguvu mpya, na kutoka katika maumivu ahadi ya muqawama wa kiraia wenye heshima, kutoka katika kumbukumbu ya watoto, tujenge daraja kuelekea mustakabali ambao ndani yake hakuna mtoto atakayefedheheshwa, hakuna mama atakayevunjika moyo, na hakuna matumaini yatakayozikwa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha