Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh “Nazim Al-Saidi”, mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Nujabaa na Naibu Katibu Mkuu wa harakati hiyo, katika kongamano la “Ahadi ya Uthabiti; kutoka subira hadi ushindi”, huku akirejelea nafasi ya muqawama nchini Iraq, alisisitiza kwamba; hataruhusu nchi hiyo kuwa uwanja wa mahesabu ya maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akiashiria kwamba Hashd al-Shaabi na muqawama haviwezi kutenganishwa, alisema: Tutamjibu kwa jibu kali yeyote atakayeivamia heshima ya watu wa Iraq.
Sheikh Nazim Al-Saidi katika sehemu nyingine ya hotuba yake aligusia mjadala wa usimamizi wa silaha nchini Iraq na kusema: Tunatumaini kwamba yale yanayojadiliwa bungeni kuhusu mpango wa serikali na suala la kuhodhi silaha yatakuwa ya kiuhalisia na yatakayohudumia maslahi ya taifa la Iraq, ikiwa makusudio ya “silaha zisizo chini ya udhibiti” ni silaha za uvunjifu wa sheria na machafuko, basi hilo halihusiani na silaha za wapiganaji wa muqawama; kwa sababu wao katika mazingira magumu zaidi wamekuwa watetezi wa maeneo matakatifu na watu.
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Nujabaa huku akisisitiza msimamo thabiti wa harakati hiyo tangu mwanzo hadi sasa, alikumbusha kuwa: Sisi hatukuingia katika mfumo wa kisiasa na bunge, bali tunasimamia mwenendo wa utoaji huduma kwa watu wa Iraq, licha ya mabadiliko ya hali na mazingira, tutabaki pale tunapopaswa kuwa; pembeni mwa watu, maeneo matakatifu na misingi yetu, na tutaendelea kuwa imara katika njia ya muqawama.
Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake akiwaelekea wapambanaji wenzake na wanasiasa waliotokana na muqawama, alisema: Muqawama si kwa silaha pekee, bali pia ni kusimama kwa msimamo, kutoa huduma na kuwa waaminifu. Watu ambao siku moja katika vita dhidi ya ugaidi waliwasimamia nyinyi katika mabonde na milima, leo wanatarajia kutoka kwenu aina nyingine ya muqawama; muqawama dhidi ya ufisadi na pia kupambana na uzembe na kutofanya kazi kwa ufanisi ambako kunaharibu ndoto za vijana wetu.
Maoni yako