Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika ujumbe wake amesema: Nguvu za kibeberu daima zimekuwa na viwango vya pande mbili kuhusiana na utawala haramu wa Kizayuni; Siku ya Nakba ambayo kwa kila Mpalestina haijaleta chochote isipokuwa uharibifu, ukimbizi, mauaji na misiba, ni siku ambayo ndani yake taifa moja na maelfu ya familia zilivunjika, mauaji ya kimbari ya kiwango kikubwa pamoja na ukatili wa kinyama yalitokea; lakini kwa upande mwingine, siku hiyo hiyo huadhimishwa kama “Siku ya Kimataifa ya Familia.”
Katika ujumbe huo imeelezwa: Zaidi ya miongo saba iliyopita, utawala haramu wa Israel ulipandikizwa kama kisu chenye sumu ndani ya moyo wa Mashariki ya Kati, na tangu wakati huo hadi sasa, mataifa madhlumu ya eneo hili na hata nchi jirani yamekuwa wahanga wa njama na sera za upanuzi za utawala huo wa Kizayuni pamoja na waungaji mkono wake wa kikoloni.
Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan ameendelea kusema: Hata nguvu za kibeberu zinazounga mkono utawala huo leo hazijasalimika kutokana na athari za njama zao wenyewe, na vita walivyovilazimishwa dhidi ya Iran vimewatumbukiza katika tope zito; tope ambalo ni matokeo ya sera hizo hizo za uvamizi na kuunga mkono utawala wa Kizayuni.
Mwanazuoni huyo mashuhuri wa dini amesisitiza kuwa: Siku ya Nakba kwa kila Mpalestina na kila mwanadamu huru mwenye dhamiri ni kumbukumbu ya majanga ya kibinadamu, mauaji, ukimbizi na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu; siku ambayo majeshi ya uvamizi na makundi yenye silaha ya Kizayuni yaliwafukuza takriban Wapalestina laki saba na elfu hamsini kutoka katika nyumba zao, ardhi zao na maeneo yao ya kuzaliwa, na dhulma hii ya kihistoria bado inaendelea.
Ameongeza kusema: Iraq, Syria, Lebanon, Somalia na nchi nyingine za eneo hili hazikudhoofishwa kwa mabomu pekee, bali pia kupitia njama za ndani, na kulifanyika jaribio la kueneza wigo wa vita hivyo hadi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; vita ambavyo kwa hakika ni sehemu ya mradi wa “Israel Kubwa” na sera za utawala wa Kizayuni. Pamoja na hayo, taifa la Iran licha ya kutoa viongozi mashahidi na kujitolea mhanga mkubwa, bado limesimama kama ukuta wa chuma mbele ya adui.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi mwishoni amesema: Mkanganyiko wa wazi wa nguvu za dunia uko hapa kwamba kwa upande mmoja wanaitaja tarehe 15 Mei kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Familia, lakini kwa upande mwingine wananyamaza mbele ya uharibifu na kuangamizwa kwa familia za Kipalestina na mataifa ya eneo hili. Maadamu mkono wa dhulma wa Uzayuni na ubeberu wa kimataifa hautadhibitiwa, amani na usalama wa kudumu duniani havitapatikana.
Maoni yako