Jumapili 17 Mei 2026 - 13:00
Kuitegemea Marekani haijawahi kuwa njia ya wokovu wala haitakuwa hivyo kamwe

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Muin Daqiq, katika mkusanyiko mkubwa wa wanazuoni wa Hawza na Umma wa Hizbullah, huku akisisitiza kuwa; ushindi wa kambi ya haki ni jambo la uhakika, aliwataka watawala wa Bahrain wachukue funzo kutokana na hatima ya wale wanaotegemea ubeberu, na akaeleza kuwa; njia ya wokovu imo katika kushikamana na Qur’ani na umoja wa Umma wa Kiislamu, si Marekani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Muin Daqiq, mwakilishi wa Hizbullah ya Lebanon mjini Qum, katika mkusanyiko mkubwa wa wanazuoni wa Hawza na Umma wa Hizbullah uliofanyika usiku uliopita katika ukumbi wa Imam Khomeini (r.a) ndani ya Haram tukufu ya Hadhrat Ma’sumah (a.s), huku akitegemea Aya za Qur’ani Tukufu, alielezea kuwa; sunna ya Mwenyezi Mungu katika kuwasaidia Waumini haiwezi kukiukwa, na akirejelea ahadi za Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani alisema: Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, maadui wa Uislamu daima wamekuwa wakijaribu kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu ataitimiliza nuru Yake hata kama makafiri watachukizwa.

Akaongeza kusema: Nusura na ushindi ni ahadi ya lazima ya Mwenyezi Mungu kwa Waumini, ikiwa mtakuwa na subira na msimamo, na mkabaki thabiti katika njia ya haki, Mwenyezi Mungu atakusaidieni na atawadhalilisha maadui, hatima ya madhalimu siku ya kiyama haitakuwa chochote isipokuwa hasara na adhabu.

Onyo kwa watawala wa Bahrain na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi

Mwakilishi wa Hizbullah ya Lebanon mjini Qum katika sehemu nyingine ya hotuba yake, huku akirejelea hali nyeti ya nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi, hususan Bahrain, aliwaambia watawala wa nchi hizo kwa kusema: Chukueni funzo kutoka katika historia, kuiegemea Marekani au nguvu za kigeni hakujawahi kuwa njia ya wokovu wala hakutakuwa hivyo kamwe.

Muqawama ni utekelezaji wa kivitendo wa ahadi za Mwenyezi Mungu

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Muin Daqiq, huku akikumbusha mafanikio ya muqawama nchini Lebanon na Palestina, alisisitiza: Yale tunayoyaona leo katika medani za muqawama ni utekelezaji wa kivitendo wa ahadi za Mwenyezi Mungu, kama ambavyo muqawama ulipata ushindi dhidi ya utawala wa Kizayuni, ndivyo pia imani ya mataifa ya eneo hili mwishowe itawashinda madhalimu.

Kuifanya upya ahadi kwa mashahidi wa muqawama na uongozi

Aidha aliendelea kwa kuadhimisha kumbukumbu na majina ya mashahidi wa muqawama, hususan shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, na kusisitiza: Sisi tunashikamana na ahadi yetu kwa Walii Faqihi na viongozi wa muqawama, na tunaweka wasia wa mashahidi wakubwa kuwa nuru ya njia yetu, hakuna shinikizo lolote, iwe Bahrain au sehemu nyinginezo, linaloweza kuyumbisha irada ya Umma wa Kiislamu ambao umefungamana na Qur’ani na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s).

Kuwa macho dhidi ya njama za uchochezi wa mifarakano; njia ya wokovu imo katika umoja

Mwakilishi wa Hizbullah ya Lebanon mjini Qum mwishoni aliwataka watu wa mataifa ya eneo hili kuwa macho mbele ya njama za kuchochea mifarakano, na akasema: Njia ya wokovu imo tu katika kushikamana na mafundisho ya Qur’ani, kufuata madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s), na kuwa na umoja chini ya mhimili wa muqawama, inshaallah kwa msaada wa Mwenyezi Mungu ushindi wa mwisho utaandikwa kwa ajili ya wanyonge katika ulimwengu huu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha