Jumamosi 16 Mei 2026 - 14:00
Ayatullah al-Udhma Subhani amthamini muuguzi aliyeyaokoa maisha ya watoto wachanga nchini Iran

Hawza/ Hadhrat Ayatullah Subhani, huku akitoa shukrani kwa juhudi za jamii ya sekta ya afya, alisema: Niliona picha za kujitolea mhanga kwa muuguzi aliyekuwa akiwaokoa watoto wachanga; aliumba tukio ambalo ni kazi ya malaika.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, sambamba na Wiki ya Kitaifa ya Afya, Daktari Abrazeh, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Qum, pamoja na wajumbe wa baraza la uongozi wa chuo hicho, walikutana na Hadhrat Ayatullah Subhani, mmoja wa Mar'aji wakubwa wa taqlidi.

Hadhrat Ayatullah Subhani katika kikao hicho, huku akitoa shukrani kwa juhudi na kazi za jamii ya sekta ya afya nchini, alisisitiza: Kujitolea mhanga kwa jamii ya sekta ya afya katika Vita vya Kulazimishwa vya Ramadhani ni jambo lenye thamani na litakalobakia milele.

Kiongozi huyo alisisitiza juu ya jambo hili kwamba; madaktari, wauguzi na wahudumu wa tiba katika vita hivi vya karibuni walikuwa miongoni mwa nguzo za ushindi na nguvu ya taifa la Iran.

Marji' huyo wa taqlidi aliongeza: Niliona picha za kujitolea mhanga kwa muuguzi aliyekuwa akiwaokoa watoto wachanga; aliumba tukio ambalo ni kazi ya malaika.

Daktari Abrazeh, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Qum, naye pia katika kikao hicho aliwasilisha ripoti kuhusu hatua za chuo hicho na shughuli za jamii ya sekta ya afya ya mkoa huo, hususan katika Vita vya Tatu vya Kulazimishwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha