Jumamosi 16 Mei 2026 - 12:00
Ni mwanadamu aliyejirekebisha pekee ndiye anayeweza kurekebisha wengine

Hawza/ Baraza la Vijana wa Harakati ya Kiislamu chini ya uongozi wa Sheikh Sayyid Ibrahim Yaqub Zakzaky katika eneo la Fentua (eneo la Sayyid Zakzaky), limefanya mkusanyiko wa kielimu na kitamaduni wa siku mbili kwa lengo la kubadilishana mawazo na kutoa mafunzo katika mji wa Tudun Aya.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Vijana wa Harakati ya Kiislamu katika eneo la Fentua, limehitimisha hatua ya mwisho ya kongamano lake kubwa la kikanda ambalo lilikuwa linafanyika katika mji wa Tudun Aya.

Sheikh Ashiru Abdullah Fentua katika hotuba ya kufunga kongamano hilo aligusia karibu mada zote zilizowasilishwa katika kipindi chote cha kongamano, na akatoa nasaha kwa washiriki na jamii kwa ujumla.

Kuhusu ufisadi na hali mbaya zilizopo katika jamii pamoja na juhudi za Sayyid Zakzaky za kuirekebisha jamii, alisema: “Mwenyezi Mungu amempa ilhamu kiongozi wetu kwamba ufisadi huu lazima urekebishwe, na kwa kuwa lengo ni kurekebisha maovu haya, ni lazima watu watembee katika njia ile ile ambayo Mtume Mtukufu (s.a.w.w) aliwafundisha masahaba wake; kwa sababu hakuna anayeweza kuwa mrekebishaji isipokuwa yule ambaye yeye mwenyewe amesharekebishwa.”

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, aliwahimiza washiriki kujitegemea na alisema: “Kuwepo katika njia ya mapambano na harakati ya Kiislamu kunahitaji roho ya kujitosheleza; kwa sababu katika maisha haya, fitna nyingi na tofauti hutokana na haja kubwa ya mwanadamu. Wakati mtu anaposhindwa kujikimu kwa mahitaji yake, hulazimika kuwaomba wengine, na hili ni aina ya udhalili kwa mwanamume na mwanamke.”

Pia kuhusu kuzingatia mavazi ya Kiislamu na kuhifadhi hijabu kwa mujibu wa maamrisho ya Sharia, alisema: “Bila shaka kuzingatia sheria ya Mwenyezi Mungu katika suala la hijabu kamili na mavazi yenye staha, huilinda jamii dhidi ya kuangukia katika ufisadi na uchafu ambao leo umeenea katika jamii. Mavazi yasiyofaa na uzembe katika hijabu ni miongoni mwa sababu kuu za kuongezeka kwa ufisadi wa maadili duniani.”

Mwishoni mwa hotuba yake, aliwataka watu kuwa na umoja na kujiepusha na mifarakano, na alisema: “Miongoni mwa njama za maadui ni kwamba hawataki kamwe Umma wa Kiislamu uwe na umoja. Daima matamanio yao ni kuleta tofauti baina ya Waislamu; kwa sababu tukikuwa na umoja na mshikamano, tutakuwa na nguvu, na wao watakuwa dhaifu.”

Katika sehemu nyingine ya programu hiyo, kabla ya hotuba ya kufunga, Ustadh Nura Isa Bakori katika hotuba yake yenye anuani: “Maadili; njia muhimu zaidi kwa vijana katika kufikisha ujumbe wa Harakati ya Kiislamu”, alianza kwa kusisitiza maadili mema na kusema: “Hakuna kitu kinachomkurubisha mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu na kuwafanya watu wampende kama maadili mema.”

Aliendelea kusema: “Jihadi ya nafsi maana yake ni kupambana na nafsi yako na kuirekebisha; jihadi hii ni kubwa zaidi na ngumu zaidi kuliko jihadi ya upanga. Kama vile mwili wa mwanadamu daima unavyohitaji chakula, roho ya Muumini nayo daima inahitaji chakula cha kiroho; chakula ambacho huijenga na kuitakasa roho. Wakati roho ya mwanadamu inapokuwa safi na yenye afya, mwanadamu hupambwa kwa maadili ya Mitume na walinganiaji wa Mwenyezi Mungu. Ikiwa umeweza kujibadilisha mwenyewe, unaweza kuwabadilisha wengine pia; lakini ikiwa wewe mwenyewe hujarekebika, basi kuwarekebisha wengine ni jambo lisilowezekana.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha