Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Kashan Iran, Mojtaba Raee katika kikao chake na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Iraq mjini Isfahan, huku akielezea uwezo wa kihistoria, viwanda, utalii na kielimu wa manispaa hiyo, alitangaza utayari wa Kashan kwa ajili ya kupanua ushirikiano wa pamoja na miji ya Iraq katika nyanja za uwekezaji, usafirishaji wa bidhaa nje, elimu ya juu na uhusiano wa miji.
Meya wa Kashan, huku akieleza uwezo mbalimbali wa mkoa aa Kashan alisema: Mkoa huu hii wenye miji saba na vijiji 58 upo katika njia ya barabara kuu ya Isfahan–Tehran na una nafasi muhimu ya kimkakati.
Raee pia alirejelea uwezo wa kiuchumi wa mkoa huo na kuongeza: Kuwepo kwa forodha huru na usafirishaji wa kila mwaka wa bidhaa wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 250, kumeandaa mazingira mazuri kwa ajili ya kuendeleza biashara na nchi ya Iraq, pia eneo maalumu la kiuchumi linalojengwa litaunda fursa mpya kwa uwekezaji wa viwanda na madini.
Meya maalumu wa Manispaa ya Kashan, huku akirejelea mambo ya pamoja ya kitamaduni na kidini kati ya Iran na Iraq alisema: Kuwepo kwa Sharifu Sultan Ali bin Muhammad Baqir (a.s), shughuli zaidi ya 1000 za kidini, na uwepo wa mawakibu 15 kutoka Kashan katika matembezi ya Arubaini, kumeunda uhusiano wa kina wa kitamaduni na kidini kati ya mataifa mawili.
Raee aliendelea kwa kuashiria uwezo wa kielimu wa Manispaa hiyo na kusema: Kuna vituo 15 vya elimu ya juu vyenye zaidi ya wanafunzi 25,000 katika Manispaa hii, na takribani wanafunzi 3000 wa Iraq pia wanasoma katika ngazi za elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Kashan.
Meya wa Kashan, huku akitangaza utayari wa Kashan kwa ajili ya kusaini mikataba ya ushirikiano na miji ya Iraq, alisema: Kuna utayari wa kufanya Kashan na mji wa Najaf kuwa miji dada, kupanua usafirishaji wa mazulia, maji ya waridi, dawa za mimea, machipukizi ya waridi Muhammadi, zafarani, samaki wa mapambo na kadhalika, pamoja na kurahisisha uwekezaji wa pamoja na kupanua ushirikiano wa vyuo vikuu na elimu.
Aliongeza: Uwepo wa kampuni 48 za maarifa ya kisasa na kampuni 100 za teknolojia mjini Kashan umeandaa uwezo wenye thamani kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano wa kiteknolojia, viwanda na elimu kati ya Iran na Iraq.
Maoni yako