Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Shahidi Sayyid Ali Khamenei amejibu istiftaai kuhusu “Wajibu wa maamuma iwapo Imam atasoma vibaya”, istiftaa ambayo tunaiwasilisha kwa wapenda maarifa kama ifuatavyo:
Wajibu wa maamuma iwapo Imam atasoma vibaya
Swali:
Ikiwa Imam wa jamaa katika swala atasoma kimakosa Qir'an kwa kusahau, na katika hali hiyo akaendelea na swala yake, je, katika swala zinazofuata inajuzu kuiona swala yake kuwa sahihi na kuswali nyuma yake, au ni lazima kwanza ithibitike kwamba katika swala zinazofuata atasoma kwa usahihi na kwa namna sahihi?
Jibu:
Katika swala zinazofuata inajuzu kuswali nyuma yake. Hata hivyo, ikiwa maamuma atagundua kosa la Imam katika kisomo, anaweza (kwa namna ambayo haisababishi kubatilika kwa swala yake) kumfahamisha Imam ili asahihishe kosa hilo; vinginevyo, anapaswa kufanya niya ya kuswali peke yake (furada) na ajisomee yeye mwenyewe kisomo hicho.
Maoni yako