Jumatatu 4 Mei 2026 - 08:15
Diplomasia ya Papa Francis ilikuwa na kipaumbele dhahiri kuelekea mazungumzo na ulimwengu wa Kiislamu

Hawza/ Dkt. Chiara Ferro, mwanachama wa kitivo cha sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Naples nchini Italia, katika kongamano la pili la kielimu lililokuwa na anuani isemayo “Daraja kati ya dunia, kujenga amani”, alisema kuwa; Papa Francis aliifafanua upya diplomasia ya Vatikani kwa mtazamo wa kimataifa, na safari zake za kihistoria kwenda Misri na Iraq, zikiwemo kukutana kwake na Ali al-Sistani, ilikuwa hatua muhimu katika njia ya amani na maridhiano.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kongamano la pili la kimataifa la kielimu “Daraja kati ya dunia, kujenga amani” liliandaliwa na ofisi ya dini na madhehebu ya kitengo cha mawasiliano na kimataifa cha Hawza, kwa ushirikiano na Taasisi ya Kielimu na Utafiti ya Imam Khomeini (rh), Jamiat al-Zahra na ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Vatikani, siku ya Alhamisi tarehe 30 April.

Katika mkutano huo, Dkt. Chiara Ferro, mtafiti na mwanachama wa kitivo cha sayansi ya siasa kwenye Chuo Kikuu cha Naples “Federico II” nchini Italia, alichambua nafasi ya Papa Francis katika mazungumzo ya kidini ndani ya eneo la Ghuba ya Uajemi.

Akiashiria nafasi ya kimkakati ya Asia ya Magharibi kama kitovu cha dini na tamaduni, alisema: Uwepo wa Wakristo katika eneo hili ulianza kabla ya Uislamu, lakini kwa sasa ni wachache.

Dkt. Ferro aliongeza kuwa: Diplomasia ya Vatikani katika kipindi cha Papa Francis imekuwa ya mchanganyiko wa vipengele vya kidini, kisiasa na kitamaduni, na imeweka kipaumbele bayana kwenye mazungumzo na ulimwengu wa Kiislamu.

Mhadhiri huyu wa Chuo Kikuu cha Naples alizitathmini safari za kihistoria za Papa Francis kwenda Misri na Iraq pamoja na mkutano wake na Ali al-Sistani kuwa ni hatua za msingi katika kujenga amani na maridhiano, na akasema: Papa Francis aliukumbusha ulimwengu kwamba; rehema na heshima ya kila mwanadamu na uwepo wa Roho Mtakatifu miongoni mwa wafuasi wa dini zote vinaendelea kuwepo.

Alisisitiza kuwa; mazungumzo ya dini mbalimbali hayamaanishi kufanya mapatano juu ya misingi ya kiitikadi, bali ni njia ya kuishi pamoja na kuelewana kwa pamoja.

Katika hitimisho la hotuba yake, Dkt. Ferro huku akirejelea uungaji mkono kwa wachache kwenye kidini na heshima ya utu wa binadamu kama mihimili mikuu ya mtazamo wa Papa alisema: Pope Francis aliifafanua upya diplomasia ya Vatikani kwa mtazamo wa kimataifa, na safari zake zimeimarisha mazungumzo ya dini mbalimbali katika eneo la Ghuba ya Uajemi na Asia ya Magharibi; na mazungumzo hayo bado ni muhimu na hayakwepeki kwa ajili ya kujenga mustakabali jumuishi na wenye haki.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha