Jumapili 26 Aprili 2026 - 00:00
Kiongozi mwandamizi wa Hizbullah: Mazungumzo ya moja kwa moja ya sasa ni “mazungumzo ya kudhalilisha na ya kufedhehesha”

Hawza/ Mahmoud Qomati alitangaza upinzani wake mkali dhidi ya aina yoyote ya mazungumzo ya moja kwa moja na adui Muisraeli, na akasema kuwa; mazungumzo hayo yanapingana na sheria ya kumpiga marufuku adui wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mahmoud Qomati, naibu mwenyekiti wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah na waziri wa zamani wa Lebanon, katika kauli zake alitangaza upinzani wake mkali dhidi ya aina yoyote ya mazungumzo ya moja kwa moja na adui Muisraeli, na akasema kuwa; mazungumzo hayo yanapingana na sheria ya kupiga marufuku adui wa Kizayuni na kupambana naye, na yanampa mvamizi aina fulani ya utambuzi wa kisiasa usiokubalika.

Alibainisha kuwa; adui Muisraeli anajaribu kutumia mazungumzo ili kulazimisha lengo lake kuu; yaani kuuvua silaha muqawama na kumaliza nguvu ya kuwazuia nchini Lebanon.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Hizbullah alisisitiza kwamba; badala ya mamlaka ya Lebanon kutumia mafanikio ya muqawama na msimamo wake kama karata ya nguvu ya kitaifa, imekuwa ikiziangalia silaha za muqawama kana kwamba ziko nje ya mfumo wa sheria. Muqawama ulivumilia kwa muda wa miezi 15 kwenye kuiunga mkono serikali na chaguo lake la kidiplomasia, lakini katika kipindi hicho kila siku ulilipa gharama kwa damu, huku mamlaka ikielekea kwenye maamuzi yanayokinzana na muqawama.

Mahmoud Qomati alisisitiza kuwa; mazungumzo ya moja kwa moja ya sasa ni “mazungumzo ya kudhalilisha na ya kufedhehesha”, kwa sababu yanafanyika bila Lebanon kuwa na kipengele chochote halisi cha nguvu.

Alieleza kuwa; chaguo sahihi ni mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja; kama ilivyokuwa hapo awali katika makubaliano ya kusitisha mapigano na upangaji wa mipaka ya baharini. Alifafanua kuwa; mazungumzo ya moja kwa moja yana maana ya kumtambua adui Muisraeli, jambo ambalo halikubaliki kabisa, ilhali mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yanahifadhi msimamo wa mamlaka na taifa.

Naibu mwenyekiti wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah alisisitiza: uvumilivu huu umefikia mwisho, na muqawama hautarejea tena katika sera ya kunyamaza mbele ya uvamizi wa kila siku na ukiukaji unaoendelea wa Israel.

Pia alisisitiza kuwa; muqawama utaendelea na shughuli zake hazitasimama isipokuwa kwa kupatikana uhuru kamili, si kwa ahadi au makubaliano yasiyokamilika.

Aliongeza kwa kusema kwamba; hatutakubali mpango wowote unaoendeleza uwepo wa adui katika ardhi ya kusini au unaolazimisha hali mpya, na akasisitiza: hatutakubali kuuza kusini mwa Lebanon, na muqawama utaendelea hadi kukomboa kila kipande cha ardhi ya Lebanon.

Kiongozi huyo mwandamizi pia alibainisha kuwa; Iran haikukubali Lebanon iachwe peke yake katika shinikizo, na imesisitiza kuwa usitishaji mapigano unapaswa kujumuisha nyanja zote, si kuiacha Lebanon peke yake katika uwanja wa makabiliano.

Aliongeza kuwa; ikiwa usitishaji mapigano utamalizika na hautaongezwa, basi makabiliano yataanza tena kwa uwazi, kwa sababu kusitisha mapigano pekee hakutoshi, na lengo halisi ni uhuru kamili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha