Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, shule mbalimbali nchini Tanzania zimealikwa kushiriki katika shindano maalumu la uchoraji shindano ambalo litawahusu wanafunzi wa shule za msingi tu.
Lengo kuu na dhumuni la kuwekwa kwa shindano hilo ni kuenzi kumbukumbu ya wanafunzi 168 waliopoteza maisha yao huko Minab nchini Iran katika shule ya Shajarat Twayyibah, kufuatia shambuluo la kikatili lililofanywa na utawala wa Marekani pamoja na mshirika wake Israel, shindano hilo linalenga kukuza matumaini, huruma na maadili ya kiroho kwa watoto ulimwenguni kote.
Shindano hili maalumu na la kipekee litawahusu wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita, vile vile kituo hicho kimeagiza kwamba; kila mchoro uwe na jina la mwanafunzi, darasa lake na shule husika anayosoma.
Mwanafunzi anaweza kuwasilisha mchoro halisi au picha yake yenye ubora mzuri kupitia WhatsApp namba +255 625 560 570.
Washindi 30 watapata zawadi maalumu ambazo zimeandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania pamoja na vyeti.
Mwisho wa kuwasilisha picha hizo ni siku ya Jumanne, tarehe 27 Aprili 2026.
Maoni yako