Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 21 Farvardin 1405 (10 April 2026) zilizofanyika katika Muswala wa Quds mjini Qom Iran, huku akiadhimisha siku ya arubaini ya shahada ya Imam wa Umma, alisema: Kiongozi shahidi wa Mapinduzi alikuwa mbeba nuru ya matarajio ya kweli ya kudhihiri kwa Walii wa zama (a.j), na alikuwa na mtazamo wa kuijenga nchi kwa msingi wa Ahlul-Bayt (a.s), na nuru hiyo bado inaendelea kung’aa.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kusema: Kiongozi shahidi wa Mapinduzi alionesha kwamba; manaibu wa kweli wa Imam wa Zama (a.j) katika kila zama ni wale wanaochukua hatua kwa moyo wote katika kutekeleza malengo ya Ahlul-Bayt (a.s). Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi kuhusu Imam shahidi alisema: “Kiongozi wetu shahidi alikuwa faqihi mwenye utambuzi wa zama na mujahidi mwenye basira asiyechoka.”
Aliongeza kusema: Shahada ya Imam wa Umma kwa upande mmoja, na kuchaguliwa kwa Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi kwa upande mwingine, kunakumbusha riwaya zinazohusiana na manaibu maalumu wa Imam wa Zama (a.j) katika kipindi cha ghaiba ndogo. Katika zama hizo, baba na mwana walipata heshima ya kuwa manaibu maalumu. Baada ya kufariki kwa Uthman bin Saeed Amri ambaye alikuwa naibu wa kwanza wa Imam wa Zama (a.j), Imam wa zama (a.j) alimchagua mwana wake Muhammad kuwa naibu maalumu wa pili. Uchaguzi huu haukutokana na urithi au wasia wa baba, bali ulitokana na ustahiki wa mwana huyo.
Imam wa Ijumaa wa Qom aliongeza: Baada ya shahada ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Baraza la Wataalamu wa Uongozi kwa niaba ya watu na kwa kuzingatia sifa alizokuwa nazo Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, lilimteua kuwa Walii Faqihi na naibu wa jumla wa Imam wa Zama (a.j) na kumtangaza kwa wananchi.
Akiashiria kwamba taifa la Iran ni mtengeneza historia, alisema: Taifa la Iran ni ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu, ambayo kwa mujibu wa baadhi ya kauli, Mwenyezi Mungu ameahidi kuwaleta katika Suratul-Maida:
«یَا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا مَنْ یَرْتَدَّ مِنْکُمْ عَنْ دِینِهِ فَسَوْفَ یَأْتِی اللَّهُ بِقَوْمٍ یُحِبُّهُمْ وَیُحِبُّونَهُ»
Enyi mlioamini! Atakayeacha dini yake miongoni mwenu, basi Mwenyezi Mungu ataleta watu ambao Yeye anawapenda nao wanampenda.
Aliendelea kusema: Mwenyezi Mungu katika aya hii anataja sifa za kundi hili na anasema:
«أَذِلَّةٍ عَلَی الْمُؤْمِنِینَ أَعِزَّةٍ عَلَی الْکَافِرِینَ یُجَاهِدُونَ فِی سَبِیلِ اللَّهِ وَلَا یَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ذَٰلِکَ فَضْلُ اللَّهِ یُؤْتِیهِ مَنْ یَشَاءُ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِیمٌ»
Kwa waumini ni wanyenyekevu na wanyonge, na kwa makafiri ni wenye nguvu na heshima; wanajitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa mpana na Mwenye kujua yote.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Fatima Ma’suma (a.s), akieleza kuwa kuna uwezekano kuwa walengwa wa aya hii ni taifa shujaa la Iran, alisema: Hili ni jambo la kujivunia; taifa la Iran limebadilisha mlinganyo wa nguvu na limegeuka lenyewe kuwa dola kubwa yenye nguvu, na wananchi wameazimia kuihifadhi nguvu hili kwa ajili ya kuinua neno la Mwenyezi Mungu.
Alisema: Imam shahidi wa Umma kuhusu watu hawa alisema: “Iwapo jambo lolote litatokea katika nchi hii, Mwenyezi Mungu atawainua watu hawa”; leo dunia inashuhudia kuinuka kwa watu na kutohofia kwao shahada. Taifa la Iran limeinuliwa ili kumfedhehesha na kumuangamiza Firauni wa zama kwa irada ya Mwenyezi Mungu.
Mwakilishi wa Walii Faqihi katika mji wa Qom alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika ujumbe wa tarehe 20 Farvardin alisema: “Hakika sauti zenu katika viwanja zina athari katika matokeo ya mazungumzo.” Na akatoa bishara kwamba: “Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kutokana na mchango huu na kuendelea kwake, upeo unaolikabili taifa la Iran unaashiria kudhihiri kwa zama tukufu, zenye mwangaza, zilizojaa heshima, utukufu na ustawi.”
Aliongeza: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuhusu hamasa ya taifa la Iran alirejea ushindi wa taifa hilo katika vita ya tatu ya kulazimishwa, na akasema: “Leo dalili za kuinuka kwa Jamhuri ya Kiislamu kama nguvu kubwa na kushuka kwa ubeberu kuelekea udhaifu zimekuwa wazi mbele ya macho ya wote. Hii bila shaka ni neema ya Mwenyezi Mungu.”
Imam wa Ijumaa wa Qom alisisitiza: Ashura ya Huseini ni ramani ya njia kwa Iran, na siku hizi ni Ashura inayojirudia; kwa msingi huo taifa la Iran kwa kufuata mwenendo wa Imam Hussein (a.s) katika kukabiliana na Yazidi wa zama, hupaza sauti ya “Hayaath minadh-dhilla” (Hatutakubali udhalili). Kwa kaulimbiu na uelewa huu, taifa la Iran daima limegeuza maombolezo kuwa hamasa. Mara hii pia limegeuza maombolezo ya shahada ya Imam wa Umma kuwa hamasa kubwa kiasi cha kumshusha Trump mcheza kamari kutoka katika ile sura yake ya kutisha ya bandia. Taifa la Iran limethibitisha kwa ulimwengu utekelezaji wa kauli: «یدالله فوق ایدیهم».
Wosia kwa taasisi wanadiplomasia
Akiielekezea hotuba yake kwa taasisi ya diplomasia alisema: Kama vile majeshi yetu yanavyolenga shabaha zao kwa usahihi wa hali ya juu (kupiga kwa nukta maalumu), vivyo hivyo maafisa wa diplomasia wanapaswa kulenga kwa umakini huo huo, wasionshe udhaifu wowote, na wachukue dhamana na uhakika wa kutosha mbele ya makubaliano yoyote ambayo maadui wenu wanaingia.
Aliendelea kusema: Imam Ali (a.s) katika maagizo yake kwa Malik al-Ashtar alisema:
Baada ya kufanya sulhu na adui, uwe makini sana na tahadhari; kwa sababu wakati mwingine adui hukaribia ili kukushitukiza. Hivyo basi uwe mwenye kuona mbali na uwe na tahadhari juu ya adui.
Mwakilishi wa Walii Faqihi katika mji wa Qom alisisitiza kuwa: Haifai kabisa kumdharau adui wa leo mwenye tabia ya mbwa mwitu. Majeshi yetu katika uwanja wa mapambano na umma huu shujaa mitaani “wameipatia Iran heshima na kumdhalilisha adui.” Taasisi ya diplomasia nayo inapaswa kuifikisha Iran kwenye heshima na kumshusha adui mdanganyifu kwenye udhalili.
Akiwa pia anatoa pole kwa msiba wa shahada ya Imam Ja‘far as-Sadiq (a.s), alisema: Imam as-Sadiq (a.s) amesema:
«أیما مُؤمِنٍ نَفَّسَ عَن مُؤمِنٍ کُربَةً وهُو مُعسِرٌ یَسَّرَ اللّهُ لَهُ حَوائجَهُ فی الدُّنیا والآخِرَةِ»
Muumini yeyote anayemwondolea muumini mwenzake dhiki ilhali yeye yuko katika hali ya uhitaji, Mwenyezi Mungu humrahisishia mahitaji yake katika dunia na Akhera.
Kulinganisha mazingira ya Sulh al-Hudaybiyyah na hali ya jamii ya leo
Ayatullah Saeedi katika khutba ya kwanza alisema: Kuzingatia taqwa kuna athari nyingi, miongoni mwake ni kuzuia madhara ya adui. Madhara makubwa ya adui si ya mali tu, bali ni madhara ya hadhi, ya kiroho na ya kidini. Mwenyezi Mungu katika Suratul Aal Imran anasema:
«وَإِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا یَضُرُّکُمْ کَیْدُهُمْ شَیْئًا»
Ikiwa mtavumilia na kuwa wachamungu, hila zao hazitawadhuru kwa lolote.
Alisema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 17 ya Suratul-Fath anawataja wale ambao jukumu la jihadi limeondolewa kwao, akisema:
«لَیْسَ عَلَی الْأَعْمَیٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَی الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَی الْمَرِیضِ حَرَجٌ وَمَنْ یُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ یُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِی مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَنْ یَتَوَلَّ یُعَذِّبْهُ عَذَابًا أَلِیمًا»Hakuna lawama kwa kipofu, wala kwa kilema, wala kwa mgonjwa [iwapo hawatashiriki katika vita]. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, atamwingiza katika mabustani ambayo mito inapita chini yake; na anayepuuza, atamuadhibu kwa adhabu chungu.
Imam wa Ijumaa wa Qom alieleza kwamba ili kuielewa aya hii, ni lazima kwanza kuelewa muktadha wa jumla wa sura hii, kwa kuwa inahusiana na tukio kubwa la kihistoria na la malezi, nalo ni Sulh al-Hudaybiyyah. Alisema: Wakati Mtume (s.a.ww) alipokwenda Makka pamoja na kundi la Waislamu kwa ajili ya kufanya Umra, makafiri wa Kiquraysh waliwazuia njiani na hawakuwaruhusu kuingia Makka. Hapo hapo katika eneo la Hudaybiyyah, walikozuiwa Waislamu, sulhu ilifanyika baina ya Waislamu na makafiri.
Aliendelea kusema: Sulh al-Hudaybiyyah kwa mtazamo wa awali ilikuwa kama kurudi nyuma kwa Waislamu, kwa sababu baadhi ya masharti yake yalikuwa kwa manufaa ya makafiri wa Kiquraysh; lakini Qur’ani imeutaja mkataba huu kuwa ni ushindi ulio wazi. Jambo hili kwa kiasi fulani linafanana na hali ya sasa ya Iran.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom aliongeza: Mwenyezi Mungu alionesha kwamba; katika mkataba huu ambao kwa nje ulionekana kuwa wa kuzuia, kulikuwa na upeo mpana zaidi wa kuenea kwa Uislamu. Moja ya mihimili muhimu ya sura hii ni uchambuzi wa makundi mbalimbali ya jamii ya Kiislamu mbele ya tukio la Hudaybiyyah.
Alisema: Katika tukio hili, Waislamu waligawanyika katika makundi manne. Kundi la kwanza ni waumini waliokuwa na imani thabiti na waliokuwa na yakini kamili katika ahadi ya Mwenyezi Mungu, waliomsindikiza Mtume (s.a.ww) na wakafanya bay‘a ya uaminifu katika Bay‘at al-Ridwan.
Kundi la pili ni wanafiki na wale waliokuwa na shaka juu ya ahadi ya Mwenyezi Mungu, wakidhani kwamba Waislamu hawangerudi salama kutoka safari hiyo; lakini baada ya kurejea kwa Mtume (s.a.ww), walitoa visingizio na kumwomba msamaha. Kundi la tatu ni wale wenye udhuru katika uwanja wa vita, ambao aya ya 17 inawahusu.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Fatima Ma‘suma (a.s) alisema: Mwenyezi Mungu katika aya hii anaweka wazi mpaka kati ya udhuru wa kweli na visingizio. Katika Uislamu, jukumu huwekwa kwa kadiri ya uwezo wa mtu. Mwenyezi Mungu anatukumbusha kuwa hatupaswi kuruhusu tofauti za uwezo na mitazamo kusababisha mpasuko wa kijamii. Jamii ni kama mwili mmoja; ikiwa kundi fulani haliwezi kuwepo mstari wa mbele kwa sababu fulani, haimaanishi kuwa limeacha njia. Kwa subira na huruma, ni lazima kuimarisha safu ya ndani mbele ya shinikizo la nje, kiuchumi, kijeshi, kitamaduni na mengineyo.
Alibainisha: Shahada katika utamaduni wa Kiislamu, hasa katika siku hizi ambazo tumeshuhudia shahada ya Imam wa Umma, makamanda, wasomi, wananchi wa kawaida na wanafunzi wa shule ya Shajarat Tayyibah, imekuwa ni mtihani mkubwa.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qom alisema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 17 ya Suratul-Fath anaeleza kwamba ushindi na kufunguka (fat-h) hupatikana chini ya kivuli cha kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata uongozi wa umma. Katika aya hii, Mwenyezi Mungu anawapa bishara Waislamu kwamba kila anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ataingia Peponi.
Aliongeza kuwa: Vilevile Mwenyezi Mungu katika aya hii anaeleza kwamba; katika nyakati ambazo kunakuwa na hali za kipekee zinazofanya hukumu fulani kubadilika, kuna watu wanaotafuta kutumia vibaya hali hiyo ili wajihesabu miongoni mwa wenye udhuru. Mwenyezi Mungu anawatahadharisha watu wa aina hiyo.
Mwakilishi wa Walii Faqihi Qom alikumbusha kuwa: Hata leo, sisi tunasikiliza na kufuata amri za Walii Faqihi wa jamii, Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, ili nasi tupate kunufaika na ushindi huu ulio wazi.
Maoni yako