Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Swala ya maiti juu ya mwili mtukufu wa Imam Shahidi na mashahidi wa familia yake iliongozwa asubuhi ya jana (Jumanne, 16 Tir 1405 H.Sh.) na Hadhrat Ayatullah Jawadi Amuli, huku ikihudhuriwa na umati wa mamilioni ya wapenzi wa Kiongozi Shahidi katika Msikiti Mtukufu wa Jamkaran.
Wakati wa kuongoza swala hiyo, Hadhrat Ayatullah Jawadi Amuli alishindwa kujizuia kutokana na majonzi; koo lake lilibanwa na hisia, macho yake yakajaa machozi, na machozi yake yakamtiririka kwa majonzi ya kuondokewa na Imam Mujahid wa Umma.
Ushuhuda Ayatullah al-Udhma Jawadi Amuli kwa Kiongozi wa Umma
Hadhrat Ayatullah Jawadi Amuli, alipokuwa akiongoza Swala ya maiti juu ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alitoa maelezo ya juu kabisa na muhtasari wa sifa za kipekee za Imam Shahidi katika sehemu za mwisho za swala hiyo kwa mfumo wa ushuhuda, ili ubaki milele katika historia.
اللَّهُمَّ إِنَّ هذَا الْمُسَجَّی قُدّامَنَا، عَبْدُکَ وَ ابْنُ عَبْدِکَ وَ ابْنُ أَمَتِکَ
Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika huyu aliyelazwa mbele yetu ni mja Wako, mwana wa mja Wako na mwana wa kijakazi Wako.
نَزَلَ، نَزَلَ، نَزَلَ بِعِزِّ جَلَالِکَ وَ جَبَرُوتِکَ وَعَظَمَتِکَ وَ مَلَکُوتِکَ
Ameshuka, ameshuka, ameshuka mbele ya utukufu, adhama, nguvu kuu, ukubwa na ufalme Wako.
نَزَلَ بِعِزِّ جَلَالِکَ وَ جَبَرُوتِکَ وَ مَلَکُوتِکَ
Ameshuka mbele ya utukufu, adhama, nguvu kuu na ufalme Wako.
نَزَلَ بِعِزِّ جَلَالِکَ وَ جَبَرُوتِکَ وَ مَلَکُوتِکَ
Ameshuka mbele ya utukufu, adhama, nguvu kuu na ufalme Wako.
اللَّهُمَّ إِنَّهُ نَزَلَ مُجاهِداً، مُبالِغاً، وَرِعاً، مُوَحِّداً، مُتَأَلِّهاً
Ewe Mwenyezi Mungu! Amekuja Kwako akiwa mujahidi mwenye kujituma kwa hali ya juu, mchamungu, mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na mwenye kumtambua Mola wake.
اللَّهُمَّ، اللَّهُمَّ، اللَّهُمَّ، إِنَّهُ نَزَلَ عِنْدَکَ شَهِیداً لِلْإِسْلَامِ وَ الْقُرْآنِ وَالْعِتْرَةِ؛ هذَا أَوَّلاً
Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika amekuja Kwako akiwa shahidi kwa ajili ya Uislamu, Qur'ani na Ahlul-Bayt; huu ndio ushahidi wetu wa kwanza.
اللَّهُمَّ، اللَّهُمَّ، اللَّهُمَّ، إِنَّهُ نَزَلَ عِنْدَکَ قَتِیلاً لِلْإِسْلَامِ؛ قَتِیلاً لِلْأُمَّةِ الْمُسْلِمَةِ؛ قَتِیلاً لِسِیَاسَتِهَا؛ قَتِیلاً لِصِیَانَتِهَا؛ قَتِیلاً لِکِیَانِهَا؛ قَتِیلاً لِعَظَمَتِهَا وَ سِیَادَتِهَا وَ مَوْلَوِیَّتِهَا وَ وَحْدَتِهَا
Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika amekuja Kwako akiwa aliyeuawa katika njia ya Uislamu; aliyeuawa kwa ajili ya Umma wa Kiislamu; aliyeuawa kwa ajili ya siasa ya Kiislamu; aliyeuawa kwa ajili ya kuulinda Uislamu; aliyeuawa kwa ajili ya kulinda uwepo na mamlaka ya Umma; aliyeuawa kwa ajili ya utukufu wake, uongozi wake, Wilayah yake na umoja wake.
یَا مَنْ یَقْبَلُ الْیَسِیرَ وَ یَقْبَلُ الْیَسِیرَ، اقْبَلْ مِنْهُ وَ مِنَّا الْیَسِیرَ، إِنَّکَ عَلَی کُلِّ شَیْءٍ قَدِیرٌ
Ewe Yule unayekubali hata amali ndogo na kuilipa kwa malipo makubwa! Kubali kutoka kwake na kutoka kwetu amali hii ndogo; hakika Wewe ni Muweza juu ya kila kitu.
اللَّهُمَّ إِنَّهُ نَزَلَ بِعِزِّ غُفْرَانِکَ، وَ هُوَ عَبْدُکَ وَ مُحْتَاجٌ إِلَی رَحْمَتِکَ
Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika amekuja chini ya hifadhi ya utukufu wa msamaha Wako, naye ni mja Wako na mwenye kuhitaji rehema Zako.
اللَّهُمَّ احْشُرْهُ مَعَ الْأَئِمَّةِ الْهُدَاةِ الْمَهْدِیِّینَ
Ewe Mwenyezi Mungu! Mfufue pamoja na Maimamu waongozaji na walioongoka.
وَاخْلُفْ عَلَی أَهْلِهِ فِی الْغَابِرِینَ، صَلِّ عَلَیْهِ وَ عَلَیْهِمْ أَجْمَعِینَ، وَاحْشُرْنَا مَعَهُ مَعَ عِنَایَتِکَ وَ عِنَایَةِ مُحَمَّدٍ وَ عِتْرَتِهِ الطَّاهِرِینَ
Na uwajaalie wema na ulinzi wale aliowaacha nyuma yake; mteremshie rehema yeye na wote hao; na utufufue pamoja naye kwa uangalizi Wako na kwa uangalizi wa Muhammad na Ahlul-Bayt wake watoharifu.
Kubusu kilemba cha Bwana wetu Kiongozi Shahidi
Marjii huyu wa Taqlid pia, kabla ya kuongoza Swala ya maiti, alikibusu kilemba cha Sayyid wetu Kiongozi Shahidi; busu lililotokana na ikhlasi safi na mapenzi ya dhati yaliyotoka moyoni.
Maoni yako