Jumatano 8 Julai 2026 - 15:32
Ka'dhimayn Yapokea Miili Mitukufu ya Familia ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hawza/ Mji mtukufu wa Ka'dhimayn nchini Iraq umejawa na hali ya huzuni na majonzi baada ya kupokea miili mitukufu ya familia ya Mtukufu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika hatua ya kuendelea kwa taratibu za kuwaaga na kuwaheshimu viongozi hao waliopoteza maisha.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, miili mitukufu ya familia ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ilifika katika mji wa Kadhimayn asubuhi ya leo, Jumatano, ambapo waumini na wananchi walijitokeza kwa wingi kutoa heshima zao za mwisho na kushiriki katika hafla ya mapokezi ya miili hiyo mitukufu.

Kadhimayn, ambayo ni miongoni mwa miji mitakatifu ya Iraq na wenye kumbukumbu kubwa ya kielimu na kidini, umegeuka kuwa eneo la maombolezo na kumuaga, huku waumini wakionesha mapenzi yao na mshikamano wao kwa familia ya kiongozi huyo shahidi.

Mapokezi hayo yamefanyika katika mazingira ya huzuni kubwa, huku washiriki wakisoma dua, kutuma salamu za rambirambi na kueleza heshima zao kwa maisha, juhudi na mchango wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na familia yake katika kuhudumia dini na umma.

Baada ya mapokezi hayo, miili hiyo mitukufu inatarajiwa kuendelea na safari ya kuagwa katika maeneo mengine matakatifu, ambapo waumini watapata fursa ya kushiriki katika ibada za maombolezo na kutoa heshima zao za mwisho.

Tukio hili limekuwa sehemu ya kumbukumbu kubwa inayowakutanisha waumini na wafuasi wa Mapinduzi ya Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali, katika kuenzi maisha na misimamo ya Kiongozi Shahidi na familia yake.

Ka'dhimayn Yapokea Miili Mitukufu ya Familia ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha