Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ammar Hakim siku ya Jumatano alipokea kwa furaha kusitishwa kwa mapigano katika vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na akasisitiza umuhimu wa kuheshimu mamlaka ya nchi na kutokikiuka uhuru huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake ya habari, Sayyid Ammar al-Hakim alitoa wito wa kuwepo kwa umakini na uhalisia katika mazungumzo yajayo kati ya Iran na Marekani, na akaeleza matumaini yake kuwa; mazungumzo hayo yatafikia amani ya kudumu na yenye uthabiti katika eneo hili, yatazuia kujirudia kwa matukio kama hayo, na kuwalinda watu wa eneo hilo, wakiwemo wa Iraq, dhidi ya majanga ya vita na athari zake za uharibifu.
Maoni yako