Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya Qom iliyofanyika Ijumaa tarehe 14 Farvardin 1405 (4 April 2026) katika Msikiti wa Muswalla Quds wa Qom, alisema: Leo taifa la Iran liko mstari wa mbele katika busara na uchambuzi sahihi ndani ya uwanja.
Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini Iran alibainisha: Tuko katika hali nyeti sana katika historia ya Uislamu na katika hatua ya kipekee mno ya mabadiliko yenye utukufu ya Jamhuri ya Kiislamu na historia ya eneo na Ummah. Taifa kubwa la Iran, uongozi mkuu, vikosi vya kijeshi, na taasisi zote za Iran ndio wabeba bendera na vinara wa njia hii, ambao waliinua bendera yenye ukubwa wa historia nzima na wakaumba muujiza usio na mfano.
Imamu wa Ijumaa wa Qom alisisitiza kwamba: Tunapomtazama adui katika hatua hii nyeti ya kihistoria na tukio hili muhimu, tunaona makosa kadhaa ya kimahesabu aliyofanya. Dunia haikuwahi kudhani kwamba wao, pamoja na vyombo vyao vya uchambuzi na rasilimali kubwa walizonazo, wangeingia katika makosa ya kimahesabu. Katika vita na katika kazi zote kubwa, usahihi au makosa ya kimahesabu ni jambo muhimu sana.
Kosa la Kwanza
Alisema kwamba: Walidhani kwamba Iran na taifa la Iran, kutokana na matatizo na tabu zilizopo, wangekata tamaa, wangeshindwa na kupoteza uwezo wa kusimama imara na kufanya uchambuzi sahihi katika mapambano mazito.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kusema: Wao waliweka msingi wa vita vyao juu ya hesabu potofu kuwahusu nyinyi; kwa sababu taifa letu kwa namna ya kimiujiza lilikuwepo uwanjani, lilipata uchambuzi sahihi na kutambua njia sahihi, hata katika hali ambayo lilikuwa likishuhudia misiba mingi.
Aliongeza kwamba; busara na ujasiri wa watu wa Iran viliharibu hesabu zao: Uelewa wao wa jamii ulikuwa dhaifu na dhaifu sana. Taswira yao kuhusu utamaduni na taifa letu ilikuwa potofu. Waliona kwamba taifa hili ni lile lile la miaka minane ya kujihami kwa utakatifu (vita vya kujihami) na zama za Mapinduzi ya Kiislamu. Ushiriki huu umeunda mfano mpya wa muqawama. Lazima iandikwe nadharia mpya ambayo msingi wake ni uwepo, uelewa, busara na ujasiri wa taifa.
Mkurugenzi wa Hawza za kielimu aliongeza kusema: Katika vita, watu huingia mafichoni na muundo wa mataifa huvunjika, lakini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, muundo wa taifa hili leo ni imara zaidi kuliko wakati wowote. Na Trump mwendawazimu ajue kwamba; taifa hili litasimama kwa uthabiti zaidi kuliko wakati mwengine wowote katika uwanja wa muqawama.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom alisema: Swala za Ijumaa na uwepo wa kila usiku katika mitaa yetu vinaonyesha uimara huu wa kitaifa na nguvu ya imani.
Kosa la Pili
Mjumbe wa wanazuoni wa Baraza la viongozi aliongeza kusema: Adui alidhani kwamba; kwa pigo moja kubwa mfumo wa kisiasa wa Iran ungeporomoka. Kwa dhana hiyo, aliwakusanya mamluki, akapanga mikakati muhimu, akafanya shambulio la kushtukiza na akawaua kishahidi watu wakubwa. Hata hivyo, hili lilikuwa kosa, kwa sababu mfumo huu wa kisiasa una mizizi katika nafsi na imani ya taifa, na hakuna tofauti kati ya watawala na wasiokuwa watawala.
Aliendelea kusema: Kinyume na walivyodhani, mfumo wetu wa kisiasa uliendelea kuwepo, na taasisi zote zilirekebishwa kwa haraka na mbadala ukawekwa. Katika kilele cha hatua hizi kulikuwa na Amiri Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi ambaye taasisi ya Wataalamu wa Uongozi (Majlisi ya Khobregan) ilirekebisha kwa haraka. Urekebishaji huu wa haraka na uwekaji wa mbadala ni miongoni mwa fahari za mfumo wetu wa kisiasa.
Ayatullah A‘rafi alisema: Leo pia tunasema kuwa; taasisi zetu zote zimepanga hatua kadhaa za baadaye. Pigo lolote mtakalopiga, mbadala utakuja na mfumo utarekebishwa. Mfumo wetu wote wa kisiasa ni imara, na licha ya chuki za Trump, Netanyahu na maadui wa Iran, taasisi zote pamoja na uongozi viko katikati ya uwanja na viko tayari kwa mapambano.
Mkurugenzi wa Hawza alisema kuwa: Chipukizi mpya zinakuja kwa kasi. Waliwaua kishahidi makamanda wa anga na anga za mbali, lakini leo makamanda wenye nguvu zaidi wapo. Waliwaua kishahidi viongozi wa kijeshi, kisiasa na kijamii, lakini badala yao kuna kizazi kipya. Hii ni sura mpya ya kung’ara kwa vijana katika medani ya vita na mapambano. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hii.
Kosa la Tatu
Aliendelea kusema kuwa: Walidhani kwamba Iran iko katika nafasi ya kujihami na itabaki katika nadharia zake za zamani za kujilinda, na kwamba kwa pigo moja la haraka itaanguka. Hata hivyo, nadharia yetu ya kijeshi na mkakati wetu wa kimapambano umebadilika, na subira ya kimkakati ya miongo kadhaa mbele ya mamluki na vituo vyao katika eneo imefika mwisho, na ramani yetu imebadilika.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom alikumbushia kwamba: Kwa zaidi ya miongo minne, tumepokea mapigo kutoka kwa mamluki hawa na vituo vya adui katika eneo, lakini kwa ajili ya umoja na maslahi tulivumilia. Hata hivyo, leo nadharia yetu ya ulinzi ni ya kushambulia. Vita vyetu ni vya kikanda na ikiwa itahitajika vitakuwa vya kimataifa. Subira yetu ya kimkakati imekwisha, na katika kukabiliana na uvamizi wenu tutasimama kwa nguvu, kwa mashambulizi na tutashambulia. Taifa hili kwa mtazamo huu mpya liko tayari kusimama, kufanya jihadi na kufa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu litashinda.
Kosa la Nne
Alisema: Kosa lao la nne lilikuwa ni kudhani kwamba vita vya kawaida na silaha na viwanda vya kisasa vya kijeshi ndio msingi wa ushindi wao. Vikosi vyetu vyenye nguvu vimepiga hatua kubwa katika vita vya kawaida na teknolojia za kijeshi, kiasi kwamba leo vimeangamiza F-35 ambayo ni alama ya nguvu ya Marekani. Hata hivyo, kosa lao jingine lilikuwa kwamba vita ambavyo wao hawana zana zake viko mikononi mwetu, na huo ni Mlango wa Hormuz.
Mkurugenzi wa Hawza aliendelea kusena: Maeneo yote muhimu ya eneo yako mikononi mwa vikosi vya Uislamu na Iran, kwa vita vya kawaida na visivyo vya kawaida, na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, nguvu hii itavunja hesabu zenu katika nyanja zote.
Kosa la Tano
Alisema: Kosa jingine la maadui lilikuwa kudhani kwamba mhimili wa muqawama umevunjika na washirika wa Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu wameanguka na kwamba muungano wa muqawama haupo tena. Akili dhaifu ya Netanyahu na Trump ilifanya uchambuzi huu potofu. Walidhani kwamba mhimili wa muqawama baada ya majeraha makubwa ya miaka miwili umeangamia. Lakini hii ilikuwa ni kosa.
Imamu wa Ijumaa wa Qom alisisitiza pia: Leo mhimili wa muqawama umejijenga upya na umeinuka kwa nguvu kama mnyororo. Lebanon, Iraq, Yemen na maeneo mengine ya dunia yameinuka. Mwamko huu haukuwa ndani ya taswira zenu. Leo mhimili wa muqawama umepata uhai mpya, una chipukizi mpya na utabaki imara katika dunia nzima.
Kosa la Sita
Alibainisha pia: Walidhani kwamba watapata uungwaji mkono mkubwa duniani na NATO pamoja na nchi nyingine zitajiunga nao, lakini wengi hawakuunga mkono kwa uhalisia au hata kwa sura ya nje. Mawazo ya umma duniani yako pamoja na Iran ambayo imesimama peke yake dhidi ya nguvu zote za kiburi na inawatetea wanyonge wote wa dunia.
Kosa la Saba
Khatibu wa Ijumaa wa Qom aliendelea: Kosa jingine la kimahesabu la adui lilikuwa ni kudhani kuwa; kutatokea machafuko ya ndani, lakini hili lilizimwa kwa usalama wa ndani uliotokana na nyinyi wenyewe, uwepo wa vikosi vya polisi, Basij tukufu na watu jasiri.
Alisema: Ulinzi wetu ni wa Kimungu, wa kiimani, wa ustaarabu, wa kihistoria, wa kikanda na wa kimataifa, unaotegemea sheria ya dini, akili na sheria za kimataifa. Ulinzi wetu ni wa watu, wa kitaifa kwa ujumla, wa taasisi mbalimbali na ni muunganiko wa nyenzo zote kwa ajili ya heshima na utukufu wa taifa.
Maoni yako