Jumatano 1 Aprili 2026 - 22:20
Vita vya leo si mgogoro kati ya Iran na Marekani; ni vita kwa ajili ya haki ya dini na hatima ya Umma

Hawza/ Ayatullah Sayyid Yasin Mousawi, huku akisisitiza kwamba matukio yanayoendelea yanazidi migogoro ya mipaka, aliona kwamba; kutokuwa na upande wowote katika vita vya Ramadhani ni kuungana na batili, na akavitaja kuwa ni mwendelezo wa vita vya kihistoria vya “Imam Hussein (as) na Yazid”.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Yasin Mousawi, Imamu wa Swala ya Ijumaa Baghdad na mmoja wa walimu mashuhuri wa Hawza ya kielimu ya Najaf Ashraf, katika khutba alizozitoa siku ya Ijumaa tarehe 7 Farvardin 1405 (27 March 2026), huju akisisitiza unyeti wa matukio yanayoendelea katika eneo, alitangaza kuwa, wiki hii ni “wiki ya maamuzi katika maisha ya Uislamu na Waislamu”. Akiashiria mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya vikosi vya Al-Hashd al-Sha‘bi na jeshi la Iraq, alisisitiza kwamba; hatua hizi si tukio la kupita au mgogoro wa mipaka kati ya nchi, bali ni sehemu ya mpango ambao kwa mujibu wake unalenga kuangamiza dini ya Uislamu na kuisukuma Iraq kwenye msimamo wa kutokuwa na upande kwa sura ya nje—ambao kwa vitendo unamaanisha kuungana na kambi ya Marekani dhidi ya mkondo wa Muqawama.

Imamu wa Swala ya Ijumaa Baghdad katika sehemu nyingine ya maneno yake alirejelea “shambulio la vikosi vya Marekani na Israel dhidi ya Hashd Tukufu” na kusema kwamba; mashambulizi haya hayakulenga tu vikosi vya Hashd al-Sha‘bi, bali pia yalijumuisha sehemu za jeshi la Iraq; jambo ambalo kwa mujibu wake linaonesha kuwa misingi ya muundo wa ulinzi wa Iraq pia imelengwa.

Ayatullah Mousawi pia alikosoa msimamo wa baadhi ya taasisi rasmi za Iraq, hasa Baraza la Ulinzi wa Taifa na kusema kwamba; kusema hatua za vikosi vamizi kuwa ni “kujilinda” kwa hakika ni aina ya kuhalalisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni katika ardhi ya Iraq. Aliongeza kuwa; baadhi ya mikondo ya kisiasa inajaribu kuwasilisha yanayoendelea kama ni “vita kati ya Iran na Marekani au Israel” tu, na kuionesha Iraq kuwa nje ya mlinganyo huu; ilhali, kwa mujibu wa simulizi hii, Baghdad inapaswa kutokana na uhusiano na makubaliano yake na Tehran na Washington kubaki karibu na “pande zote mbili”.

Imamu wa Swala ya Ijumaa Baghdad katika muktadha huu, huju akirejelea mfano wa kihistoria, alisema; mtazamo huu unafanana na ule unaosema katika riwaya za kihistoria kwamba “Sayyiduna Hujr bin ‘Adi aliuawa na Sayyiduna Mu‘awiya”; simulizi ambayo kwa mtazamo wake ni aina ya kuunda pande mbili kati ya haki na batili. Aliongeza kuwa mtazamo huu kwa hakika ni ule ule wa kuiona Marekani na Iran kama pande mbili zilizo sawa, ilhali “kutokuwa na upande” huku kwa vitendo kunamaanisha kujiondoa katika vita kati ya haki na batili.

Akiuliza swali kwamba chanzo cha msimamo huu ni nini?!, alitaja uwezekano kama utegemezi, maslahi ya kifedha au kuitegemea Marekani, lakini akasisitiza kwamba; hana nia ya kumtuhumu mtu maalumu, bali anapinga kuafikiana kwa msimamo rasmi wa Iraq na simulizi ya Marekani.

Ayatullah Mousawi aliendelea kusisitiza kuwa: Iraq si uwanja tu wa mashindano ya kisiasa, bali ni “Qibla ya Ushia”; kwa sababu kaburi tukufu la Amir al-Mu’minin Ali(as)، kaburi la Imam Hussein(as) na pia makaburi ya Maimamu wanne miongoni mwa Maimamu Ma‘sumin (as) yapo katika ardhi hii. Alisema kwa hiyo, vita vya sasa si kati ya nchi au mipaka, bali ni vita juu ya ukweli wa Ushia na dini ya Mtume wa Uislamu (saww) ambayo kwa mujibu wake wanazuoni wa fiqhi wamekuwa wabeba bendera wake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha