Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Isa Qasim, kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Bahrain, alitoa tamko ambalo ndani yake alitoa rambirambi kwa kuuawa kishahidi kwa kijana wa Bahrain, Sayyid Muhammad Mousawi, ambaye ameuawa kishahidi chini ya mateso mabaya katika jengo la uchunguzi wa jinai linalohusiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain.
Sheikh Issa Qasim katika tamko lake lililochapishwa na “Tovuti ya al-Muqawim”, alieleza kwamba; mwanadamu muumini miongoni mwa raia wa Bahrain, kwa mtazamo wa sera rasmi ya nchi hii na kwa ajili ya kupata ridhaa ya Marekani, hana tena thamani hata ya uzito wa mdudu chungu au mbu; na kumkatakata na kuuvunjavunja mwili wake hali akiwa hai, na kufa kwake chini ya mateso makali, hakuchukuliwi ila kuwa ni chombo cha kujifurahisha na kupata ridhaa ya “wanyonyaji wa damu za watu wema duniani.
Aliongeza kuwa: Hili la kwamba mja mwema wa Mwenyezi Mungu, Sayyid Muhammad Mousawi na mfano wake wanateswa katika njia ya kuitumikia dhulma ya kimataifa, liko mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu, na watu wa Bahrain hawatasahau dhulma walizofanyiwa.
Sheikh Issa Qasim mwishoni alimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aongeze malipo ya baba mtukufu wa shahidi, familia yake adhimu, waumini wa Bahrain na mataifa yaliyo hai na yenye imani.
Maoni yako