Jumatano 1 Aprili 2026 - 18:20
Barua ya Ayatullah A‘rafi kwa kiongozi wa Orthodoksi wa Urusi; Laani jinai za kinyama zinazofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni

Hawza/ Ayatullah A‘rafi katika barua aliyomwandikia Patriarki Kirill, kiongozi wa kiroho wa Kanisa la Orthodoksi la Urusi, ametaka kulaaniwa kwa jinai za kinyama za Marekani na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, likinukuu Ofisi ya Dini na Madhehebu ya Naibu wa Masuala ya Kimataifa ya Hawza, Ayatullah A‘rafi katika barua aliyomwandikia Patriarki Kirill, kiongozi wa kiroho wa Kanisa la Orthodoksi la Urusi, huku akionesha huzuni kubwa kutokana na kuuawa kishahidi kwa Marji' Mkuu katika ulimwengu wa Kishia na kulipuliwa kwa shule ya wasichana huko Minab, ametaka kulaaniwa kwa jinai za kinyama za Marekani na utawala wa Kizayuni.

Mkurugenzi wa Hawza katika barua hii alieleza kuwa; kulengwa kwa makusudi Marji' wa juu kabisa wa kidini, ni dharau ya wazi kwa dini zote za Mwenyezi Mungu na ni hatari ya kutisha kwa viongozi wa kiroho duniani, na akamtaka Patriarki Kirill, pamoja na kulaani jinai hii, achukue msimamo wa kibinadamu kuhusu mauaji ya watoto wasio na hatia huko Minab na atoe onyo kuhusu hatari ya kutishiwa viongozi wa kidini.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha