Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Al Mayadeen TV ikinukuu kutoka kwenye uhusiano wa vyombo vya habari vya Hizbullah kwamba: Sheikh Naeem Qassem amesema kuwa: "Haijawa siri tena kwa mtu yeyote kwamba; kuna mpango hatari kutoka Marekani na Israel unaojulikana kama 'Israel Kubwa'. Mpango huu unategemea uvamizi na upanuzi kutoka Furati mpaka Nile, ikiwa ni pamoja na Lebanon. Uvamizi wa Israel na Marekani dhidi ya Lebanon haukukoma tarehe 27 Novemba 2024, na adui wa Israel hakushikamana na makubaliano, bali aliendelea na uvamizi wake kwa muda wa miezi kumi na mitano mfululizo."
Ima Kusalimu Amri au Kupinga Wavamizi
"Sasa imefahamika kuwa tunakabiliwa na chaguo mbili: Ima kusalimu amri na kuachana na ardhi yetu, heshima, mamlaka, na mustakabali wa vizazi vyetu, au kupitia muqawama na mapambano dhidi ya wavamizi, kuzuia kutimizwa kwa malengo yao. Wakati wa kujibu uvamizi huu ulichaguliwa na muqawama ili kumzuia adui kushtukiza na kuizuia Israel kuishambulia Lebanon pekee. Pia, ulighairi madai yote ya kisingizio, kwani kurusha roketi kadhaa haiwezi kuwa kisingizio cha vita, hasa katika hali ambapo uvamizi wa adui umedumu kwa miezi kumi na mitano."
Kuendeleza Njia ya Muqawama
"Muqawama umeandaa vifaa na maandalizi muhimu, na umethibitisha ufanisi na uwezo wake. Vijana mashujaa na wazalendo wameunda ushujaa wa uhodari, heshima, uzalendo, na utu. Wameazimia kuendelea na mapambano bila kikomo chochote na hawana kikomo cha kujitolea. Leo muqawama ni ishara ya utukufu ya uzalendo na wabashiri wa uhuru wa baadaye. Watu wa muqawama pia ni watu walio bora zaidi na wenye heshima zaidi; kama sehemu ya mchango katika juhudi za kupigania uhuru, wamevumilia maswaibu na kuwatoa kafara watoto wao kwa fahari na ridhaa. Wamevumilia kwa shida kubwa kutengwa na nyumba zao na maisha ya kawaida ili kujenga mustakabali huru na wenye heshima kwa nchi yao na watoto wao. Uvamizi ni tatizo na hatari, na muqawama ni tumaini na njia ya ukombozi. Dhima ya kukabiliana na uvamizi ni dhima ya kitaifa inayowakabili wote, ikiwa ni pamoja na serikali, taifa, jeshi, vikosi, makabila, vyama, na kila raia."
Hila ya Uvamizi na Kuikalia Lebanon
"Uvamizi wa Israel na Marekani unataka kuinyima Lebanon nguvu zake na kutawala sera na mustakabali wa watoto wake. Wanataka kuharibu mamlaka na uhuru wa Lebanon kwa kuleta fitina na migogoro ya ndani, kuhalalisha uvamizi wa Israel, na kuzuia jeshi kupewa silaha za kujilinda na nchi; na jibu la suala hili ni wajibu wa kitaifa. Linapotokea suala la kumiliki silaha pekee ili kujibu matakwa ya Israel huku uvamizi na ukaliaji ukiendelea, hiyo ni hatua inayoelekea kwenye kuiharibu Lebanon na kutimiza ndoto ya Israel Kubwa."
Mazungumzo na Adui Mvamizi Hayakubaliki
"Kadhalika, pendekezo la mazungumzo na adui wa Israel wakati wa vita, linamaanisha kukubali kusalimu amri na kuinyang'anya Lebanon uwezo wake wote; zaidi ya hayo, kanuni ya mazungumzo na adui anayekalia ardhi na kufanya uvamizi kila siku ni ya kukataliwa. Hakuna vita inayofanyika kutoka kwa wengine katika ardhi ya Lebanon; bali ni vita ya Israel na Marekani dhidi ya Lebanon ikikabiliwa na ulinzi wa muqawama, watu, jeshi, watu waadilifu, na vikosi vinavyoamini katika uhuru na ukombozi wa Lebanon. Tuko katika vita vya kujihami kwa ajili ya Lebanon na wananchi wake."
Mashahidi Ni Watu Waliochaguliwa Zaidi
"Wale wanaouawa kishahidi ni miongoni mwa waliochaguliwa zaidi kwa wanaume, vijana, wanawake, na watoto wa taifa hili, na kile tunachokikomboa ni ardhi ya nchi yetu ya Lebanon."
Umoja wa Kitaifa Utaondosha Matumaini ya Mvamizi
Tunatoa wito kwa umoja wa kitaifa dhidi ya adui wa Israel na Marekani, chini ya jina moja katika hatua hii: Kusitisha uvamizi kwa ajili ya ukombozi wa ardhi na watu. Vyeo vingine vyote vinaweza kujadiliwa baadaye. Umoja wa kitaifa utamuondolea matumaini mvamizi wetu katika kuikalia kimabavu nchi yetu. Umoja wa kitaifa utaturuhusu kupitia hatua hii ngumu kwa umoja na ushirikiano, na kujenga nchi yetu pamoja. Umoja wa kitaifa unamaanisha serikali isifanye maamuzi yanayohudumia mpango wa Israel, hata kama haikusudii hivyo, kwa sababu matokeo yatakuwa kwa faida ya Israel. Umoja wa kitaifa unamaanisha serikali irudi nyuma kutoka kwenye uamuzi wake wa kuzitangaza shughuli za muqawama na vikosi vya muqawama kuwa ni wahalifu. Tunatoa wito kwa umoja wa kitaifa kwa ajili yetu sote. Pamoja tutakuwa na nguvu zaidi na pamoja tutafupisha muda wa uvamizi huu. Tazama uvamizi wa Israel na Marekani dhidi ya Lebanon; wanauwa raia, wanabomoa majengo, wanawakimbiza watu kutoka vijijini na miji, na wanatafuta kuiharibu ardhi na vizazi, huku wakiwa wanyonge mbele ya wapiganaji shupavu wa muqawama. Muqawama huu hautashindwa, na watu na raia waadilifu wa nchi yetu wako pamoja nao. Tuna uhakika na matumaini kwamba, hatutashindwa kamwe, hata fidia itakuwa kubwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na sisi tumelitimiza ahadi kwa wale waliodhulumiwa duniani kuwafanya viongozi na warithi." Lakini kile kinachoendelea katika mapambano ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya uvamizi wa kimataifa wa Marekani na Israel ni somo la kuigwa.
Ushindi wa Iran dhidi ya Nguvu Zenye Kiburi Zaidi Duniani
Iran imesimama imara dhidi ya nguvu zenye kiburi zaidi duniani na wahalifu wake, na kwa uwezo wa Mungu itashinda. Jua kuwa kila ushindi dhidi ya Marekani na Israel unaleta kheri kwa wote: "Na ushindi hautoki ila kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima."
Maoni yako