Jumatano 25 Machi 2026 - 22:40
Watu elfu 7 Watia saini  “Ahadi ya Wanazuoni wa Hawza kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Iran” hadi sasa

Hawza/ Hadi sasa zaidi ya wanazuoni elfu 7 wa masomo ya hawza wamesaini “Ahadi ya Wanazuoni wa hawza kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu,” na mchakato huu unaendelea na unaongezeka kila wakati.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya kukusanya saini za "Ahadi ya Wanazuoni wa hawza" kwa Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, Kiongozi wa Waislamu na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, imezinduliwa kwa jitihada za Shirika la Habari la Hawza.

Hadi sasa zaidi ya watu 7,000 kutoka hawza wamesaini ahadi hii (kiaga cha utiifu) na mchakato huu unaendelea na kuongezeka kila wakati.

Wanafunzi wa dini na viongozi wa hawza wanaweza kushiriki katika harakati hii kwa kusaini na kuthibitisha ahadi hii muhimu ya kimapinduzi.

Saini ya Ahadi

Maandishi ya Ahadi ya Wanafunzi wa hawza na Viongozi wa Kidini kwa Mtukufu Imam Khamenei (Mola amuhifadhi)

Amani iwe juu yenu; tafadhali baada ya kusoma maandishi ya kiaga, zitajeni taarifa zenu binafsi kisha zithibitisheni.

Ahadi ya Wanazuoni wa Kiislamu kwa Mtukufu Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei, Kiongozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu, imeandaliwa kwa jitihada za Shirika la Habari la Hawza, na ninyi mnaweza kushiriki kwa kusaini na kuthibitisha ahadi hii.

Kwa huzuni kubwa na mioyo iliyojaa majonzi, hawza, wanazuoni, wanafunzi wa dini na waumini kwa ujumla wanatoa rambirambi kwa kupata shahada kwa “Mtukufu Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (ra),” kiongozi mwerevu na mtawala wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa Imam wa Zama (aj), Mara'ji' wakubwa wa Taqlid, wananchi watukufu wa Iran, na Umma wa Kiislamu.

Yeye alikuwa mshumaa wa uongofu katika dhoruba ya kimataifa ya dhulma na upotofu, na kwa upeo wa kimungu na uchamungu wa kimapinduzi, aliidumisha daima bendera ya Uislamu Safi wa Muhammadi (saww).

Matunda ya jihadi yake na uongozi wake wenye hekima yalikuwa ni heshima ya Iran, umoja wa Umma wa Kiislamu, na mwanzo wa harakati ya ustaarabu mpya wa Kiislamu.

Kumbukumbu na njia ya kiongozi huyo adhimu zitabaki hai daima katika nyoyo za taifa na hawza.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aiunganishe roho yake tukufu na Mtume Mtukufu (saww) na Mawalii wa Mungu, na aendelee kuliweka taifa la Iran thabiti katika njia ya uongozi wa Kiungu.

Kwa sasa ambapo Baraza la wataalamu wa uongozi, limechagua kiongozi na imam mwingine stahiki baada ya kuondoka kwa Kiongozi huyo wa umma, sisi wanafunzi wa dini na viongozi wa kidini katika hawza zote nchini Iran, kutokana na wajibu wetu wa kihistoria na kimungu, tunaona kuwa tunapaswa kufanya upya ahadi na “Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu, Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei (Zidumu naraka zake ).”

Tunaamini kwamba kuendelea kwa njia ya uongozi wa kidini ndio siri ya uimara na uthabiti wa Uislamu katika dunia ya sasa, na kwamba utiifu kwa Kiongozi wa Kidini ni dhamana ya kudumu kwa dini, uhuru wa taifa na heshima ya Uislamu, na hawza zinapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza malengo ya kimapinduzi na ustaarabu wa Kiislamu.

Saini ya Ahadi

Kwa hivyo katika kiaga na ahadi hii, tunaahidi:

1. Katika njia ya elimu, malezi ya kiroho na kueneza mafundisho ya kimungu, tutafuata maelekezo na mwongozo wa Kiongozi Mkuu.

2. Kwa ufahamu wa kina na ushiriki hai katika nyanja za kiutamaduni, kijamii na kisiasa, tutalinda urithi wa fikra na maadili wa Mapinduzi.

3. Tutaifanya hawza kuwa kitovu cha uamsho, umoja na huduma ya kiimani kwa watu.

4. Katika kukabiliana na mashambulizi ya kimataifa dhidi ya Uislamu na Uongozi wa Kidini, tutasimama kwa utetezi wa kiakili, kimaadili na kiimani.

Ahadi yetu kwa Kiongozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ni ahadi ya imani, wajibu na mapenzi ya Mungu—agano safi linalozunguka uongozi hadi kudhihiri kwa Sahibuz-Zaman (aj).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha