Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hezbullah ya Lebanon, katika hotuba yake kwa munasaba wa Siku ya Quds alisema kuwa; uvamizi wa Palestina ni dhulma kubwa zaidi ya kihistoria dhidi ya watu wa Palestina.
Alibainisha kwamba: Siku hii ina ishara na nafasi maalumu katika wito wa kuikomboa Palestina, na pia katika kueneza ujumbe huu kwa wanyonge wote duniani ili wajikomboe kutoka katika utumwa na dhulma; uvamizi wa Palestina na Baytu al-Maqdis ni dhulma kubwa zaidi katika ulimwengu wa leo.
Katibu Mkuu wa Hezbullah ya Lebanon, huku akisema kwamba; Marekani na madola makubwa ndio waliounga mkono uvamizi huu, walipanda uvimbe huu wa saratani (katika eneo hili) na mwaka 1948 wakaupa utawala huu uhalali, alisema: Vita vya sasa huko Palestina, mapambano dhidi ya adui wa Kizayuni na uhalifu pamoja na uchokozi ambao adui wa Kizayuni-Marekani anaufanya dhidi ya eneo hili na dunia, kwa hakika ni matokeo ya kupandwa huko kwa fedheha na ubaya; kupandwa kwa uvimbe huo wa saratani ambao kwa zaidi ya miaka 70 haujaruhusu eneo hili kufikia utulivu na uthabiti.
Sheikh Naim Qassem pia alisisitiza: Matokeo ya kuikomboa Palestina yatakuwa na athari muhimu kwa manufaa ya mataifa na watu; kwa upande mwingine, kuendelea kwa uvamizi wa Palestina na Quds pia kutaleta athari mbaya na madhara makubwa katika kiwango cha dunia.
Aliendelea kusema kwamba; tunapoadhimisha Siku ya Quds, maana yake ni kutangaza kwamba Wapalestina hawako peke yao na kwamba jukumu la suala hili ni jukumu la pamoja na letu sisi sote. Alisema: Watu wa Palestina wamejitoa sana katika njia hii, na katika mapambano ya mwisho dhidi ya adui wa Israeli — yaani operesheni “Tufani ya Al-Aqsa” — ndani ya Ghaza pekee zaidi ya watu 260,000 waliuawa au kujeruhiwa; mauaji ya halaiki yaliyotokea Ghaza na ambapo Israel iliharibu maisha ya watu katika eneo hilo yalifanyika kwa msaada wa moja kwa moja wa Marekani na Magharibi.
Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon aliendelea kusema: Msimamo wa Imam Khomeini (rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kuhusu Palestina ulikuwa hatua ya kihistoria ya mabadiliko, na yeye aliifanya hoja ya Palestina kuwa hai na yenye nguvu; sisi Hezbullah na muqawama wa Kiislamu tutaendelea kusimama pamoja na Palestina, tutaiunga mkono na tutawasaidia mpaka kufikia uhuru kamili.
Alisisitiza kuwa: Tunatangaza tena uungaji mkono wetu kwa Quds na kuikomboa kwake, na tunawaomba wote waungane na ukubwa huu uliodhihirika ndania ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; Iran ambayo imetoa mali zake takatifu na zenye thamani zaidi kwa ajili ya Palestina na ukombozi wake. Zawadi ya mwisho ya Iran ya Kiislamu — na zawadi ambayo bado inaendelea — ni shahada ya Ayatollah al-Udhma Khamenei ambaye alitoa nafsi yake yote muhanga na akarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na mashahidi wema kwa ajili ya lengo hili kuu na muhimu ambalo sisi sote tunapaswa kukusanyika kulizunguka.
Sheikh Naim Qassem akisisitiza kwamba; sisi huku Lebanon tuko katika vita halali vya kujilinda dhidi ya uchokozi wa kinyama wa utawala wa Kizayuni, alisema: Tunakabiliana na uchokozi wa kinyama na hatari, ambao ni tishio kwa uwepo wetu; hatukukabiliana na hali ya kawaida, bali tulikabiliana na hatua ya kinyama ambayo imeendelea kwa miezi 15. Tumewaonya mara nyingi kwamba muda unaisha, kwamba uchokozi una mipaka na kwamba subira yetu pia ina mipaka. Baada ya uchokozi dhidi ya Iran na shahada ya Imam Khamenei, tuligundua kwamba mazingira ya kukabiliana na adui huyu yameandaliwa: kwa upande mmoja, wao wamekuwa wakishambulia kwa miezi 15 na wanaonekana hawana nia ya kusitisha; kwa upande mwingine, wamemuua Imam na kiongozi wetu; na tatu, wakati mapambano yanaenda sambamba na kile kinachotokea Iran, tunaweza kumdhoofisha adui.
Katibu Mkuu wa Hezbullah ya Lebanon aliendelea kusema: Adui alianza kwa njia ya kutisha na hatari sana kuharibu nyumba, akawafanya watu wa miji yote kuwa wakimbizi kwa kisingizio cha “kupambana na muqawama”, ilhali kwa hakika wanaharibu maisha yenyewe. Hakuna suluhisho isipokuwa muqawama; vinginevyo Lebanon itaelekea kwenye maangamizi. Tunasisitiza kwamba; adui sasa hana uwezo wa kufikia malengo yake. Tumejiandaa kwa makabiliano ya muda mrefu, na watashangazwa katika uwanja wa vita. Adui ataona nguvu zetu, na vitisho vyao havitatushtua.
Maoni yako