Alhamisi 12 Machi 2026 - 13:20
Kiongozi mashuhuri wa kidini nchini Indonesia atoa bay’ah (Kiapo cha Utii) kwa Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei

Hawza/ Hujjatul-Islam Sayyid Abdullah Aridhi kutoka Indonesia katika taarifa yake ametangaza bay’ah na uungaji mkono wake pamoja na kundi la wapenzi wa Ahlul-Bayt Watoharifu (a.s.) katika mkoa wa Kalimantan Mashariki, ambao ni mji mkuu mpya wa Indonesia, kwa Kiongozi wa Waislamu, Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei (Mwenyezi Mungu amlinde).

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Abdullah Aridhi, kutoka Indonesia, mhubiri mashuhuri wa nchi hiyo, kupitia taarifa alitangaza kiapo chake cha utii na uungaji mkono wake pamoja na kundi la wapenzi wa Ahlul-Bayt watoharifu (a.s.) katika mkoa wa Kalimantan Mashariki – mji mkuu mpya wa Indonesia – kwa Kiongozi wa Waislamu, Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei (Mwenyezi Mungu amlinde).

Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Mimi Sayyid Abdullah Aridhi kutoka Indonesia, mhitimu wa shahada ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo cha Kimataifa cha Jamiatul Mustafa Al-Alamiyyah – tawi la Tehran, mhubiri wa dini na mwanzilishi wa Taasisi ya Al-Muntadhar 12 katika Kalimantan Mashariki, mji mkuu mpya wa Indonesia, kwa niaba yangu, familia yangu na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) ndani ya Kalimantan Mashariki na maeneo ya jirani, baada ya kutekeleza wajibu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema hii ya Mola na zawadi ya Kiungu kwa Umma wa Kiislamu na mhimili wa muqawama, hasa kwa taifa shujaa na tukufu la Iran, tunathibitisha uamuzi wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi katika kumtangaza Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei kuwa Kiongozi wa Waislamu, na tunatoa bay’ah yetu kwake kwa utiifu, utii na kusaidia haki, kushikamana na hukumu za Uislamu na kutii amri zake za kisheria katika kuongoza mambo ya Umma.

Tuna imani thabiti kwamba kiongozi huyu mpendwa amepewa mafanikio na msaada wa Mwenyezi Mungu na yuko chini ya uangalizi na neema maalumu ya Imam wa Zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), na tuna yakini kwamba atatembea katika njia ya haki.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mwenye Uwezo Mkubwa amlinde kiongozi huyu mpendwa dhidi ya shari za maadui wa Umma, amjaalie mafanikio katika kutekeleza majukumu yake na aimarishe hatua zake katika kuyaongoza mataifa ya wanyonge.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha