Jumatatu 16 Februari 2026 - 02:00
Kikao cha kielimu kwa anuani “Utambuzi wa kimapinduzi wa wanawake” chafanyika mjini Karachi, Pakistan

Hawza/ Kikao cha kielimu chenye anuani “Utambuzi wa kimapinduzi wa wanawake” kilifanyika kwa ushiriki wa walimu na wanafunzi katika Hawza ya wanawake ya mji wa Karachi, Pakistan, ambapo ilisisitizwa haja ya kuimarisha utambuzi, kuimarisha misingi ya kielimu na kimaadili, pamoja na nafasi ya wanawake kushiriki kwa uelewa katika jihadi ya ufafanuzi (jihad at-tabyin).

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kikao hicho cha kielimu kilifanyika kwa ushiriki wa walimu na wanafunzi katika Hawza ya wanawake ya Karachi, Pakistan. Katika mkutano huo, umuhimu wa kuimarisha utambuzi, kuimarisha misingi ya kielimu na kimaadili, na nafasi ya wanawake kushiriki kwa uelewa katika uwanja wa jihadi ya ufafanuzi vilisisitizwa.

Kusisitiza baraka za Mapinduzi ya Kiislamu katika mazingira ya kielimu na malezi
Katika hafla hiyo, Bi. Dkt. Sayyida Tasnim Zahra Mousavi, mwalimu kutoka Pakistan, katika hotuba yake huku akirejea baraka za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alieleza kuwa; mazingira ya Qur’ani, kielimu, utafiti na malezi yaliyopo katika kituo hicho cha elimu ni miongoni mwa mafanikio muhimu ya mapinduzi hayo. Alisisitiza kuwa taasisi hiyo ya kielimu ni mfano ulio wazi wa matunda ya harakati hiyo kubwa.

Dhana ya utambuzi wa kimapinduzi na umuhimu wake katika hali ya sasa Aliendelea kusisitiza umuhimu wa “utambuzi wa kimapinduzi” na kusema: utambuzi si maarifa ya juu juu tu, bali ni uwezo wa kutofautisha haki na batili, kumtambua rafiki na adui, na kusimama kwa uelewa katika njia ya uongozi (wilayah).

Mwanazuoni huyo wa dini,  huku akirejea aya tukufu isemayo: “Sema: hii ndiyo njia yangu, ninamwita Mwenyezi Mungu kwa utambuzi…”, aliongeza kuwa katika mazingira yaliyojaa fitna na changamoto za fikra na utamaduni, utambuzi wa kimapinduzi pekee ndio unaweza kuonesha njia sahihi.

Nafasi ya kihistoria ya wanawake wenye utambuzi katika mabadiliko ya Kiislamu

Aliashiria historia ya Uislamu na kusema kuwa; uwepo wa wanawake wenye utambuzi daima umekuwa na nafasi katika kubadili mkondo wa historia. Misaada ya kifedha na kiroho ya Khadija bint Khuwaylid (a.s) pamoja na hotuba na ujasiri wa Zaynab bint Ali (a.s) ni mifano iliyo wazi ya nafasi ya wanawake katika kuendeleza njia ya haki. Aliongeza kuwa; mwanamke Muislamu mwenye utambuzi ndiye mhimili wa kuendelea na kudumu kwa mkondo wa haki, na leo wanawake wenye uelewa wana nafasi muhimu katika jihadi ya ufafanuzi, kulinda maadili ya kimapinduzi na kulea kizazi kijacho. Kwa upande mwingine, adui anawalenga wanawake Waislamu kupitia vita ya fikra na utamaduni, akilenga imani, utambulisho na utamaduni wao; hivyo familia imara na wanawake wenye uelewa ni mtaji wa kweli wa kila jamii.

Katika sehemu nyingine ya kikao hicho, kulisisitizwa umuhimu wa kusoma kwa utaratibu maandiko na fikra za kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Alieleza kuwa; kusoma tafiti za Qur’ani, mijadala inayohusiana na “Hatua ya Pili ya Mapinduzi ya Kiislamu” na uchambuzi wa kihistoria wa “Mwanadamu wa miaka 250” ni muhimu sana kwa shughuli za kielimu na kitafiti za wanafunzi wa Hawza. Pia alipendekeza kurejea vyanzo vya utafiti vinavyohusiana na mada hizo, na akakumbusha kuwa; kumjunga mkono kiongozi wa Mapinduzi si kauli mbiu tu, bali ni jukumu la kiakili na kisheria.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha