Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Waziri Mkuu Datuk Seri Anwar Ibrahim alisema katika hotuba yake: “Tunataka elimu katika shule za Kiislamu iimarishwe, na kizazi cha vijana kiwekwe karibu na utajiri mkubwa wa elimu ya Kiislamu.”
Aliongeza: “Jambo hili litahakikisha kwa jamii yetu kubwa kwamba maendeleo, yanapoambatana na imani, tabia njema na hisia ya kuwajibika kwa wengine, yatakuwa maendeleo ya kweli.”
Anwar alisema: “Historia ya taifa letu haiwezi kutenganishwa na shule za Kiislamu; shule ambazo zilihifadhi imani, zililinda elimu na kuelimisha vizazi kwa ajili ya kuhifadhi utambulisho wao wakati wa utawala wa kikoloni uliopita. Ndiyo maana tunapaswa kuendelea kuimarisha elimu ya pondok na kuwaleta vijana karibu zaidi na utajiri wa elimu ya Kiislamu.”
Aidha, leo hii kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook, alisema: “Haijalishi dunia inabadilika kwa kasi kiasi gani, maendeleo huleta kheri pale tu yanapoongozwa na imani, tabia njema na hisia ya kuwajibika wengine.”
Chanzo: nst.com.my
Maoni yako